SISTER FAY AUWASHA MOTO ALIA NA WADAU
Msanii wa kike wa Muziki wa Bongoflaver na aina zake Anaetambulika kwa jina Faidha Omary ama (SISTER FAY). Anae tamba na ngoma yake mpya ya BAIYOYO, ngoma hiyo ambayo ni ya muonekano wa tofauti kulinganisha na aina ya mziki ambao aliokua akiufanya miaka ya nyuma. FAY amekua kitambo sana katika tasnia hii bila kukata tamaa toka mwaka 2006 hadi hivi leo. Kutokana na vikwazo vingi alivyopitia FAY alibahatika kutoa nyimbo kama ;- 1) NISAMEHE BABA WATOTO ambayo iliwika sana kwa mahadhi yake.. Nyingine ni 2)MJINI MIPANGO 3)SHEMEJI 4)KILIO 5)POMBE 6)KAJA MWENYEWE 7)POLE MAMA 8)MAPENZI YANAUMA 9)BILA WEWE SIWEZI Na mpaka katika karata yake ya hivi karibuni ya BAIYOYO... Ambayo video yake inaendelea kufanya vizuri SISTER FAY ameelezea vikwazo ambavyo alipitia yeye na wasanii wenzake katika kuunyanyua mziki wa Tanzania kazi ambayo ilikua sio ndogo ukizingatia wanawake waimbaji walikua hawakubaliki sana kama sasa hivi....katika jamii' Wakati akiongea na blog hii...