SISTER FAY AUWASHA MOTO ALIA NA WADAU

Msanii wa kike wa Muziki wa Bongoflaver na aina zake
Anaetambulika kwa jina Faidha Omary ama (SISTER FAY).

Anae tamba na ngoma yake mpya ya BAIYOYO,
ngoma hiyo ambayo ni ya muonekano wa tofauti kulinganisha na aina ya mziki
ambao aliokua akiufanya miaka ya nyuma.

FAY amekua kitambo sana katika tasnia hii bila kukata tamaa toka mwaka 2006 hadi hivi leo.

Kutokana na vikwazo vingi alivyopitia FAY alibahatika kutoa nyimbo kama ;-
1) NISAMEHE BABA WATOTO ambayo iliwika sana kwa mahadhi yake..


Nyingine ni

2)MJINI MIPANGO
3)SHEMEJI
4)KILIO
5)POMBE
6)KAJA MWENYEWE
7)POLE MAMA
8)MAPENZI YANAUMA
9)BILA WEWE SIWEZI
Na mpaka  katika karata yake ya hivi karibuni ya BAIYOYO...

Ambayo video yake inaendelea kufanya vizuri

 SISTER FAY ameelezea vikwazo ambavyo alipitia yeye na wasanii wenzake katika kuunyanyua mziki wa Tanzania  kazi ambayo ilikua sio ndogo ukizingatia wanawake waimbaji walikua hawakubaliki sana kama sasa hivi....katika jamii'

Wakati akiongea na blog hii 

alisema
""Nguvu nyingi jitihada ziliwarudisha chini wasanii wengi wa kike Tanzania miaka hiyo kwakua hapakua na jitihada kutoka kwa wadau za kuwasaidia....wasanii hao,"

Hata hivyo ..
Safari yake hiyo haikumkatisha tamaa,
japo kulitokea  vituo
vingi vya radio na Televishen hivyo
Mgawanyo wa kusaidia kazi na kupiga nyimbo uliegemea upande mmoja bila kuangalia wasanii waliofanya vizuri...

Changamoto la mvua ya wasanii wapya nalo liliwasahaulisha manguli wa mziki huu huku  serikali ikiwa imesahau swala zima la haki kamili..

Upenyo huo uliwafanya wadau wakajizolea marundo ya pesa kutokana na wasanii ambao wao waliambulia patupu,

Pia FAY aliipongeza serikali akasema

""Ujio wa Raisi Kikwete ulianza kufungua njia na kidogo ahueni ikatokea japo ni katika kipindi chake cha mwisho cha madaraka...
Serikali mpya nadhani italiangalia hili."".. alisema FAY

Akazidi kuksisitiza
"Bado ninaidai sanaa, bado nina malengo makubwa na sanaa...
sijakata tamaa kwani bado nina  kitu ambacho watanzania wanatakiwa wakipate .....
Hasa kuutangaza mziki wetu ki asili yetu zaidi,
Nina mipango ya kutoa ladha tofauti na zile walizosikia.. Watanzania wakae mkao wa kula
Baada ya BAIYOYO..

Pia alidokeza kua hivi karibuni ana suprise kubwa ambayo karibuni ataitambulisha ni tofauti na mziki na ni kwaajili ya mashabiki zake....

WADAU
naomba wadau ambao wapo tayari kusaidia... na kuwekeza katika mziki ninaofanya milango iko wazi
Kwa mawasiliano
INSTAGRAM @officialfaytz
(+255)679565661 ARTIST
(+255)656278685 DIRECTOR
........



Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA