IRENE :MWENYE NDOTO YA KUA ZAIDI YA JOKETI
DAR ES SAALAM: Mwanamitindo Irene Mwakalinga (22), mkazi wa Manzese Tiptop jijini Dar es Saalam amesema ndoto yake kubwa ni kuwa msanii mkubwa na mwenye mafanikio nchini kama mwanamitindo Jokate Mwegelo. …Akiwa katika pozi. Mwanamitindo huyo amezungumza hayo alipofanya mahojiano na Global Online na kusema: “Ndoto yangu ni kuja kuwa mwanamitindo mwenye mafanikio kama Jokate, najituma usiku na mchana niweze kutimiza malengo yangu. “Nia yangu kufanya vyema ndani na nje ya nchi, japo changamoto ni nyingi baada ya kufiwa na wazazi wangu, sitakata tamaa, naendelea kujituma hadi nihakikishe malengo yangu yanatimia. “Napenda kubuni mavazi, kusoma vitabu, kuangalia tamthiliya na kuchati na marafiki zangu wa karibu.” …Akifurahi jambo. Mwanamitindo huyo amesema tangu aingie kwenye sekta ya mitindo hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote. Japo usumbufu ni mkubwa kutoka kwa wanaume wenye tamaa.