JINI TUNU.. seson 1
JINI TUNU seson 1
Mtunzi... mudi bellino
Haikua mara yangu ya kwanza kwenda kwa bibi kijijini kusalimia hasa kipindi cha likizo... nilipenda sana maisha ya kijijini.... bibi aLinipenda sana alinitaka kila likizo nimtembeleee
Mara hii nilikwenda nikiwa nimesha kua mkubwa ila sikupatamani tena kijijini kama zamani.. nilikaa hata wiki haikuweza kuisha... ..
Na hii ilitokana na elimu niliofikia..na nafasi yangu kua ndogo.. maana nilikua tayari nimefika Chuo..mwaka wa 3..
Nilikuja kumtembelea Bibi yangu kwa Muda wa siku 2 tu kabla sijarudi mjini..kwa baba na mama .. Mara nyingi nikikutana na SUDI yeye pia alikuja kumsalimia Shangazi yake aliokua akiishi huku kijijini Alikua ni rafiki yangu sana ila yeye alikua anasomea ufundi magari.. na urafiki wetu ulianzia kipindi nakuja katika likizo ndefu nilipokua elimu ya msingi
...
..
...
..
Mara hii SUDI alinishawishi tukae japo siku nne maana alikua na mipango ya kutembelea.. katika nyumba za makumbusho...eneo lililokua karibu na bahari ila mbali na kijiji chetu.. Na alipanga twende nae.. Eneo lile lilikua limetelekezwa kwa muda mrefu sana lilikua kama gofu... na ilikua sehemu nzuri ya kuchukua picha kama ukumbusho... nilikubaliana na shauri lake hilo na tulipanga iwe ni moja kati ya matembezi yetu.. nililala ili niweze kuamkia safari...
....
..
.
Tulitembea mwendo kidogo..baada ya kushuka gari... SUDI alielekezwa kufika sehemu hiyo..ila ilikua mara yake ya kwanza alikua kama mimi tu sikujua chochote kuhusu gofu hilo... Tulikaribia jumba lile... kulikua na upepo mzuri sana maeneo yale.. Nyasi zilitanda katika milango na vibanda vya kupumzikia.... hakika palikua sehemu nzuri sana ya kuchukua matukio ya makumbusho..
...
..
Tulipo ingia ndani niliona vifaa mbali mbali vya mziki na vilikua vimezongwa na mabuibui.. na vumbi... kulikua na picha ukutani za watu wasioeleweka.... Huku nikitaka nimuambie SUDI turudi na tusiingie ndani yeye aliendelea nilijawa na hofu.. kwenda huku akinipa moyo kua tusiwe waoga kwani tutakua wakwanza kugundua baadhi ya vitu... na hapakua gofu kama tulivyo dhani bali jengo lilikua likitumika zamani... Mbele yangu niliona mifupa iliokua ya binadamu iliokua imejipanga katika kiti kama mtu anae soma kitabu.. ila ilikua ni mifupa tupu na kitabu kilikua mezani... huku taa mbovu iliokua kama inamulika pale katika kitabu... Nilimuonesha SUDI kwa woga.. akaniambia nisiwe na hofu... ule ni urembo tu waliokua wakiutumia watu waliokua wakiishi mule.... Tuliendelea kufungua na kufunga milango tukikata vichochoro.. vya ajabu nyumba ile kwa nje ilionekana ndogo kiasi ila tuliingia ndani kuna kona nyingi sana.... Nilivyoona kuna dalili ya kusahau tulipotoka.. nikamuamuru SUDI turudi nje... Alikubali tukaanza kufungua milango iliokua inajifunga wakati tunaingia tukiingia sisi... Tuliona kama ndio tunaenda...
...
Mara Tuliona msichana Mzuri akiwa amekaa katika kiti huku Ameshikilia gitaa...ni kama alikua anajipa burudani.. nilishangaa kumuona pale peke yake na hatukutaraji kuonana na binadamu Alitugeukia Akatuuliza kama tunatafuta mlango wa KUTOKEA...akatuelekeza... ila alituomba tujumuike mara moja katika part ya yeye na ndugu zake.. Nikamuuliza inafanyikia wapi?? Akasema nitawapeleka..SUDI alikubaki harakaharaka... Mara aliamka pale yule msichana.. akatuambia tumfate... huku nikivuta matumaini ya kua tunapata njia ya kutoka nje
: Haikua rahisi kama nilivyofikiria... Tulifika sehemu..akafungua chumba na huko tulikutana na watu wengi sana wakiwa wanafurahi.. kila mmoja alikua ameshikikia glasi yenye kimiminika che nye rangi nyekundu.. hakika haikua kinywaji cha kawaida.. kila aliekunywa alibaki na alama mdomoni kama anaekunywa rangi nyekundu... na hawakua na habari nasi.. sehemu hii ilikua kama club ya starehe.. ndani ya.lile jengo ambalo halikuonyesha dalili ya watu kukaa Tukashangaa sana.. Ghafla sikumuona SUDI nilikua mwenyewe sasa pamoja na yule dada... alinikaribisha sehemu ya kukaa na kuniuliza....
""Kinywaji gani""aliniuliza huju ananishika kidevu..
""Maji baridi"" nilijibu huku natetemeka... Watu waliokua pale wengi waliku wanawake waliovalia magauni marefu ila yalipasuliwa mgongoni hadi mabegani.. na mbele pia yalikua wazi.. walikua warembo wote walivalia viatu vya mchuchumio.... walitembea kwa madaha kwenda katika sehemu ya kuchukulia kile kinywaji chao.... Alikwenda kuniletea maji baridi.. ila wakati akiyaleta yalikua yakitoa mvuke kama yaliokua ya moto... aliniwekea na kusema
""Naitwa Tunu sijui wewe mwenzangu""
Naitwa SAM""nilimjibu huku nikiangalia yale maji fika na ule mvuke ulinipata ulikua ni wamoto.. ila nilishika ile bilauri ilikua ya baridi sana... Nikapeleka mdomoni.. maji yalipita kooni ya bariiidi ila yalipofika tumboni nilisikia ya moto.."" hali ile sikuivumilia nilipiga funda mbili nikamuambia nimetosheka... Kule ndani hakuna nilie mjua niliangaza kumtizama SUDI bila mafanikio... ""nikivunja ukimya nikamuuliza Tunu ""kwani SUDI yukwapi"" cha ajabu alicheka. Kicheko kikubwa hali ya kua mtu wa karibu lazima angegeuka ila kila mmoja alikua bize na mambo yake... Mziki uliopigwa pale sikuutambua ni waina gani maana nilisikia kengele tu na watu waliku wakiicheza... taratibu nilistaajabu kuona watu wanacheza mlio wa kengele...
Baada ya kicheko chake alinivuta na kuniwekea shavu lake kwenye shavu langu na kunionyesha kidole ..hakika nilimuona SUDI akiwa bize anasakata rumba nilishindwa kuelewa alifahamu vipi ile kengele ilikua ikigongwa kama ya kanisani.. Alikua yupo na binti mzuriii.. matumaini yalinijia nikaona tuko pamoja nae.... yule TUNU aliniletea kile kinywaji chao.. nami ninywe nilikataa.... akaniambia nimsindikize chumbani.. akabadilishe nguo avae ya mziki... nikaamka ..hadi ndani... loo kulikua pazuri sana.. alivua nguo zote na kuniacha nimeduwaa.... Alivua sidiria..taratibu kwa madaha.. na huku tulikua wawili..tu palinukia..kila kona marashi mazuri..
Alinisogelea.. hakika alikua ameumbika.. matiti yake yalisimama kama alietoka kuvunja ungo juzi..... kitovu chake alichokining'iniza kipini...macho yake mang"avu kama Paka... loo.. loo hisia zilinijia... nikaanza kumshika mwili wake uliokua mlaini kama Kambale..nikabwaga kitandani..Alipo nipa ulimi Nilihisi raha ilipokolea niliona kama kitu kimepita tumboni na kurudi.. nikaona labda ni tumbo limeshtuka..Aliponipa ulimi nilisikia raha tena ya ajabu ghafla hali ile nikaisikia tena ilikua ni kama nyoka anetambaa tumboni kwangu na yeye alining'ang'ania mdomo..wangu.. nilijichomoa kwake haraka... Loo;;; nikaona kitu kama nyoka alikirudisha mdomoni kwake... na damu zilimtapakaa mdomoni.. niliogopa nikatema mate ghafla niliona nimetema damu... Nilipo muangalia Tunu Macho yalimbadilika alianza kutoka miraba mwilini kwake kama anaepasuka roho ilinienda mbio..nikaanza kupiga kelele..alianza kuvuja damu huku ananifata nilimkwela na kuanza kukimbia.nikimuita SUDI huku nautafuta mlango wa kutokea... Ghafla akanivamia.. nilipiga kelele..
Mamaaaaaaaaaaaaa..
Nikashtuka kutoka usingizini.. bibi akiniambia..SUDI anakuita hapo nje.... Nilipatwa na hofu.. na ndoto ile Sudi alikuja kunipitia tuianze safari yetu ya kwenda katika gofu.. nilienda nje huku natetemeka nikiwaza ndoto ile ilionishirikisha mimi na SUDI..huku Akiwa amenifata kwa swala hilo hilo...
.MH
END OF SESON 1
USIKOSE
JINI TUNU seson 2
Comments
Post a Comment