JINI TUNU seson 2
ile ndoto ilinifanaya niwaze sana juu ya safari ile.. mh kwanini niliota kama vile.. nilijiuliza maswali mengi huku nikihisi kuwa hakuna kitakachoeleweka mimi na yeye katika maongezi ya SUDI.. nilitoka nje kwenda kumsikiliza...
na aliniambia kuhusu safari kwani alikua tayari amekwisha jiandaa.. na safari..
niliona si vyema kuanza kumsimulia yale yaliotokea katika ndoto ila nilimuambia kwamba sijisikii poa katika safari ile..ningehitaji kupumzika ili kesho nirudi nyumbani kwa kujiandaa na chuo ..nilijaribu kumsihi kua tuahirishe ila hakunielewa.. alinambia kua itakua si vizuri na tulibakiza siku kadhaa tu kurudi mjini..
Nilijifikiria sana ukizingatia SUDI alikua rafiki yangu tulio wasiliana katika muda wote tulipanga mengi sana mimi na yeye baada ya masomo yangu...
ilibidi nikubali nikaingia ndani kujiandaa....
Tulikunywa chai aliotayatisha bibi ..nikamuaga bibi na tukaianza safari.. huku SUDI akiwa amening'iniza kamera yake.shingoni..kwa ajili ya kuchukua kumbukumbu za matukio tuwapo safari...
gari lilitembea kwa muda mrefu sana takribani masaa ma4 mpaka tukafika.... tulishuka na Tukaanza kuifuatilia barabara ya vumbi iliokua inaingia mwituni kwaajili ya kuishika njia ya huko kunako Gofu...nyumba ya kale walioishi watu.
sikua na hofu tena kwani tayari nilikua nimeshaaizoea safari..... Tukaanza kuingia katika mazingira ya sehemu ile hakika palikua pametulia... Hofu ya kila nilichokiona katika ndoto.kilinijia.. nilitetemeka huku nikijuta na hogu ya safari yetu hii.. yote hii ikikua ni kumridhisha SUDI asijisikie vibaya ila nisingekuja huku...nilijisemea moyoni.. ilinipasa nimuambie SUDI kua Kama ikiwezekana tuishie pale pale maana nilishaliona gofu lile kwa mbali...huku moyo ukinilazimisha nisisogee ilibidi nijisingizie kua naumwa nikainama chini huku nikishikilia tumbo.... nilikaa chini kabisa SUDI alirudi nyuma na kuniuliza kipi kinanisibu ..nilimuambia kua hali yangu sio nzuri kwakua hatukua tumeachana hatua chache nilimshauri aende ila mimi ningemsubiri pale hadi atapo rudi... ila moyoni nilioana kuwa atakapoenda mimi nibaki nyuma nikimsubiri ningeondoka mbali kabisa na maeneo haya... baada ya muda kidogo.. SUDI aliondoka pale nilipokua nimekaa chini ya mti wenye kivuli kizuri... Niliogopa tu wala sikua naumwa... kwakua SUDI hakuweza kurudi kutokana tayari tulishafika Aliniamuru kua nimsubiri dk 30 anaenda kupiga jspo picha na kurudi... ili aniwahishe nyumbani alisema..SUDI na kuniacha
Nilibaki pale peke yangu..Dakika kumi zilizo pita mara alitokea mwana dada aliobebelea ungo wenye ndizi mbivu aliozioanga kama anaziuza.. akanisogelea..huku anatabasamu nikamuuliza unauza ndizi..::?
Ndio,,,, akajibu..
Nikatoa noti ya sh 500 nikampa anipe.. "" alitoa ndizi Tano akanipa... kisha aliniambia asante.. kisha akenda hatua nne siku muona akapotea kiajabu na ndizi niliziona mbele yangu.ungo mzima na ile pesa ilikua juu ya ungo nilishangaa sana hali ile sikuwahi kuona mtu akipotea mbele yangu.. duu ilikua kali.... SAM mimi kiherehere cha kuja huku na moyo ulikua hautaki..nilijuta. wakati nikiangalia huku na huku ghafla alitokea tena kama aliekua amesahau mzigo wake na kuondoka ..mara hii alipiga hatua mbili ajapotea tena..huku akiniacha mdomo wazi na hofu kedekede..... Niliamua kutaka kuondoka pale ..wakati naamka nilishikwa mkono kugeuka nilimuona yule dada amekaa kwenye jiwe nililokua nimekalia mimi kisha akaniambia ""kaa tuongee""kwa sauti nyororo kupiga kelele nilishindwa nilihisi sauti imeganda katika koo.. nilitoa neno moja tu ""kwani we nani.??..
""Akinijibu ki manjonjo na sauti legevu.. ":umenisahau??? Aliniuliza
""Mimi sikujui,, nikimjibu..
""Naitwa TUNU...akanijibu.. Nilishtuka kusikia vile jina huku kijasho kikinitoka na macho yaliokua yanatoka kwa kuogopa....mmh
END OF SESON 2
Nini kitamtokea SAM je SUDI..
USIKOSE
Comments
Post a Comment