JINI TUNU seson 3
Nilichomoka pale alipo Tunu na sikuangalia nyuma tena kwani nilihofia huenda akawa ananikimbiza...
moyo ulinirukaruka nisijue cha kufanya huku nikimuwaza SUDI kule alipo kipi kimemtokea ikiwa mimi niliokua nje ndio yamenikuta haya ..
kusema ukweli nilikimbia mbali sana kiasi kwamnb hata ile nyumba sikuiona..tena
Jua lilikua kali na sikuona.mtu
Hata mmoja.. chaajabu njia tuliokuja nayo ilinipotea na kufanya nika ingia katika muelekeo mwingine kabisa niliona kila kitu ni kipya ..niliwaza mengi niliwaza nyumbani ..niliwaza kwa bibi..
nini hichi kimenitokea.. ?? majuto yalijenga ukuta katika nafsi yangu... SAM mimi nilijionea huruma kwa jinsi nilikua natoka jasho maana niliona ni kama nime lima heka kumi kwa siku moja bila kupimzika..
nitarudi vipi nyumbani..?? nitaelekea wapi kwa wakati ule ..hakika ulikia ni mtihani wa aina yake ...
Sauti za ndege ziliniogopesha..niligeuka nyuma kila saa huku naitafuta hata alama ya vinjia vilivyotokelezea nipate kuvifuata...
Kiu ilianza kunishika nikavua begi nililokua nimevaa
ili nipate kutoa maji yaliokua ndani ya chupa...
nilipotoa yale maji nilikuta maji yamebadilika rangi nakua rangi ya damu nilitupa kihupa kile ila nolipo yatupa yaligeuka kua maji ya kawaida na kiu ilinikatika sikutaka maji tena wala sikuyachukua pale yalipo
..nikaanza kuondoka maeneo yale tena.. nilihema kwa kasi huku nakohoa na pumzi ilitaka na kuniisha .. nilihitajika kupumzika maana mwili ulikua tayari umekwisha choka.. nguvu ziliniishia.. nilitafuta sehemu yenye kivuli nikatulia....kupumzika..
Kwa mbali niliona gari likiwa linakua ila mbele yangu sikuiona njia..
nikama likikua kipita katika majani lakini lilitimua vumbia kama linalopita katia barabara...
. nililisubiri.. nikawaza likifika nilisimamishe nipande... nifanye safari ya kurudi kijijini
huku nikiwaza je SUDI itakuaje kule nilipomuacha... Nililisubiri kwa hamu basi lile huku nikilitizama kwa shauku lakini halikua linafika
Lilikua kama limesimama lakini lilikua linakuja... huku nikiwaza wanyama wale walifikaje pale ikiwa mkmi nilikua naliona gari tena likitoa moshi kabisa na mngurumo...
yalikua maajabu mengine tena..
Ghafla niliona vumbi likija ule upande niliokua nimekaa nikajua ni gari linakuja sasa..
Hee walikua ni nyati waliokua wanakuja kasi. Huku sikujua gari lile limeishia wapi... walikuja kasi kwa wingi kiasi kwamba nilijibanza na kupanda katika mti... na kuwaona wakipita chini kasi... nilihema huku nyati wale wa mwituni wakipita kama wanaohama makazi kwa kasi ..
.nikiwa juu ya mti nilishtushwa na ubaridi ulionigusa begani.. Mama yangu alikua ni nyoka aliotoa ulimi wake kule juu ya mti niliteleza kwa hofu hadi chini nikajikuta nimedondokea katika mikono ya mwanadada mrembo ni yule yule TUNU... mh...
Huyu mwanamke mbona kanifuata hadi huku.. nilijiuliza mwenyewe hatima nafsi yangu.. nilijitoa muhanga safari hii nilichomoka katika mikono yake yena kwa hasira na kumuiliza ananitaka nini kwanini anasumbua maisha yangu.. nilifoka kwa hasira
TUNU alicheka kwa dharau.. sana alicheka hadi ndege waliokua juu ya miti walikimbia kwa kicheko chake... Nilitamani aongee kua amesahau nini maana manyanyaso sio ya kitoto....na yakisha nifika shongoni.
""Aliongea neno moja tu na kusema ""wewe ni mali yangu nipo nawe popote"" kisha akapotea na sikumuona tena.... na najikuta nipo pale aliponiacha SUDI na ninaiona njia pale pale.. ghafla nikamuona SUDI akija... bila wasi wasi na kuniuliza naendeleaje.. na kuniamuru twende kwani alikua ameshamaliza....
Nilibaki kama bubu nikaongoza njia... huku mdomo ukibaki kama zoba sijui nianzie wapi kumuelezea SUDI kwa yalionitokea ...
NINI KITAENDELEA... KWA JINI TUNU
Comments
Post a Comment