JE UNAJUA KATA YA KALOLENI MOSHI KATA TAJIRI YA MALI ASILI...VIJANA WALILIA MABADILIKO

Kata ya Kaloleni inapatikana pembezoni mwa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi katika Mkoa wa Kilimanjaro. Ipo kilometa nne (4) kusini mashariki mwa Mij wa MOSHI Kaskazini imepakana na Kata ya Njoro, kusini imepakana na Kata ya Mabogini na Mashariki imepakana na Msitu wa Rau na upande wa Magharibi imepakana na Kata ya Pasua.Ina  mitaa  miwili: KALIMANI na KALOLENI, Kata inajumuisha maeneo ya makazi ambayo yamepimwa kisheria pamoja na maeneo mengine ambayo wakazi wanaishi pasipopimwa yaani Kalimani na baadhi ya eneo la Kaloleni. Kata pia imezungukwa na   ..mali asili kedekede ambao ni utajiri...wa nchi.. pia kata hii ni Kilimanjaro vew..... yaani ukiwa kata ya Kaloleni.. unauwezo mkubwa wa kuona mlima Kikimanjaro...
Ni kata yenye wakazi wapatao 5000 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002.
Kata imebarikiwa na utajiri wa mali asili.. ikiwemo chemchem.. zinazopatikana.. upande wa KUSINI maarufu kama njoro kwa GOA.. pia kumekua na mitirirko ya maji kutoka mto rau.. na chem chem iliopo upande wa Mashariki.. unaosaidia wana kaloleni kutekeleza kazi mbali mbali za kuinua uchumi.. kama kilimo cha mpunga..mbogamboga na kutumia maji hayo kama matumizi ya nyumbani.. kamwe hakuna shida ya maji hapa...
UONGOZI..
Kata ya kaloleni imekua ikipata changamoto za uongozi.. unaosahau kutekeleza ahadi na kutatua matatizo ya vijana ambao ndio changamoto za kata hii... SERIKALI imekua ikisahau kua katika kata hii kuna vijana wapatao.. 3000 wasiokua na ajira ya kueleweka... na nusu yao tayari walishaingia katika majukumu ya familia.. nakusababisha kizazi kisichokua na malengo ya maisha bora..
MABADILIKO
Vijana na wanachi wa eneo hili wameona ni vyema kabisa kuziepuka propaganda na kufanya maamuzi makali katika uchaguzi unaofuatia..
Akizungumza na blog hii... "" Kwa sharti la kutotajwa jina lake":alisema "imefika wakati sasa wananchi wa kata tajiri ya kaloleni.. kuamua maamuzi magumu ikiwa ni kubadilisha mfumo wa uongozi na kumchagua kijana atakaeweza kukumbuka idadi kubwa ya vijana wasio na ajira.. na kutufanikisha katika hili..."".kwakua vijana ndio wanaoangalia familia kwa kipindi hichi na maisha yao yamekua magumu.. tumekua hatuna ajira za kuendelea.. boda boda sio ajira ya kutuwezesha sisi tukaendeleza maisha yetu bali tunahitaji kuwezeshwa...kiuchumi.... '"alimalizia kwa kusema "" naomba vijana wenzangu mwaka huu tusifanye makosa tumchague kijana mwenzetu ili abadilishe yote haya""
ELIMU
kata ya kaloleni imekua na idadi ya kujitosheleza ya shule.. kuna shule ya Msingi kaloleni (serikali).shule ya secondary msasani(serikali)shule ya sekondary kaloleni bweni(binfsi)shule ya msingi kaloleni academic(binafsi) shule za chekechea zipatazo tatu.. hivyo ni kata pekee iliojitosheleza kielimu.. Ila serikali imekua nyuma kuiangalia kata hii..
KERO..
Kumekua na kero kedekede ikiwa ... kua na viwanda vilivyokufa toka miaka ya nyuma..ila bado vipo kama magofu.. na majengo ya kufichia ..wahalifu...
Kiwanda kidogo cha ngozi kinachotirirsha maji mchafu yanayotoa harufu...
Dampo linalotoa harufu....ikiwa taka za manispaa nzima .... kusahaulika kwa vijana wanaojitolea katika shuhuli za kijamii...
Kutokufuatilia kesi kadhaa zinazojumuisha matatizo na migogoro ya wakulima ya Mashamba.....
Serikali kuchukua maeneo ya wakulima wa zamani na kufanya ni hifadhi za misitu....
Serikali kutotekeleza swala la fidia kwa wananchi wanaoishi karibu na dampo kuu la manispaa...
MAONI..
Wananchi wanashauriwa kutoa maoni ya matatizo yao katika vyombo mbalimbali na mitandao ya kijamii ili kupaza sauti na iwafikie wahusika..
Mungu ibariki Tanzania
MUNGU ibariki KALOLENI..MOSHI..
moja ya miradi ya wnanchi ya kilimo cha mpunga....
Moja kati ya mikutano.. ya wanakijiji na viongozi wakitaka kujua hatima ya maendeleo ya kata yao
Moja ya utajiri wa maji chemi chemi za njoro kwa GOA

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA