JINI TUNU PART 6

Nilisikia mlango ukigongwa...
Kwa sauti ya ukali..... ""naani..niliuliza...
""SAM umerudiii.... Alikua ni mama amepata kurudi ..kazini... nilifungua mlango na kutoka nje...''""hee mbona Jasho?? Aliniuliza mama... ""aa mama nimekuja na kuku kutoka kwa bibi sasa si akatuponyoka Mwanao IRENE kamshika kizembe... hapa sasa hichi ni kibarua nilikua namkimbiza hata sijui kaelekea wapi..
Kama ni kuku si nimemuona bandani..":tena nikawa na muuliza IRENE huyu kuku wa nani.. maana najua hapa ndani hatuna kuku... baada ya wale kuingiliwa na ugonjwa tukawachinja wote .. ndio IRENE ananiambia kua..ni. kuku wa kaka SAM....
(Nilishangaa kwa maneno yake ya mama.. hee ilikuaje akageuka kuku tena wakati mimi nilimuona TUNU... ) sikumuonesha ishara yeyote kama kuna kilicho nitokea..."" sawa mama za huku mjini..vipi..kijijini bibi anawasalimia sana amenipa zawadi zako.. zipo kulee.. stoo.. ""umesahau mbaazi zangu..?? ""aliniuliza mama"" wee bibi alinifungia mwanzo.. anajua ugonjwa wako wewe kwa mbaazi... ""yaani nilimuambiaga hata akiona upepo unakuja mjini basi aniwekee mbaazi zinifikie.. (tulicheka na mama) ila akili yangu haikuepo pale kabisa nilifikiria yule kuku bandani....
""Mama nataka niende kilingeni kuangalia mpira.... ""basi muekee kuku chakula....ndio uondoke ""hee huyu mama vipi anania gani na mimi"" au alikua na njama na huyu kuku...""nilijisemea moyoni""
Mwambie IRENE... nilimuambia mama aliekua ndani nami nilijifanya ninaharaka nakutoka nje...""SAM ""SAM Aliita mama.. kwakua nilimuheshimu mama nikarudi hatua nyuma... ""Nimekuambia IRENE hayupo nimeshamkimbiza tution .nimekuja hapa. Namkuta bado hajaenda Tution.. ""sasa si alikua akinisubiria...nilimjibu mama.."" sasa wewe baada ya kumuambia aondoke baada ya kukuona unamuacha tu..""mama hakujua kama mimi nilijifungia chumbani nikiwa na sababu zangu..
""Haya muwekee chakula huyo KUKU kabla ya kuondoka... ""mama mpira umeshaanza"" nilimjibu kwa kudeka..""huo mpira na huyo kuku uliomleta nani muhimu... si ungemuacha tu kwa bibi yako...""au umemleta tumchinje... ""aliposema tumchinje "" niliogopa sana "" nikakimbia harakaharaka kuchukua chakula nikanyata hadi katika lile banda.. nikapenyeza mkono.. nikaingiza chakula... ""ghafla nikashikwa mkono... nikaisikia "sauti""   SAM nakuomba usimuambie yeyote kuhusu siri hii "" kisha akaniachia..
""Roho ilinipiga sana nikiwaza kuhusu huyu KUKU anaenitesa... sikujua kumbe kutoka kujijini nilimbeba TUNU na sio kuku... ""nilitoka mlangoni na kukimbia zangu kwenda kuangalia mpira...
Hofu juu ya kuteswa na jini huyu maisha yangu yote ..ilinijia..
....
...

. Nilifika kilingeni Timu yangu ilikua imeshinda goli moja sikua hata na furaha hata chembe.. japo watu walikua wakipiga kelele kwa furaha... sikuwa pale kabisa...maana niliwaza juu ya TUNU...
Hasa ulipofika muda ambao nilitakiwa kurudi nyumbani.. niliona kama ninaeenda motoni.... nilikata shauri nikaenda zangu nyumbani..  nilipokua nje niliisikia sauti ya baba ndani..
Nilitambua sasa baba alikua amerudi... nikaingia ndani nikamsalimia..
""Shikamoo baba.. ""marahaba SAM vipi za kijijini huko bibi yako anasemaje..?? ""anawasalimia ""pia kaniambia nikukumbushe juu ya paa lake sasa linahitaji kubadilishwa matundu yalijaa kila sehemu...""sawa nilikua nina wazo hilo pia.. ""mwezi ujao nitakwenda kurekebisha.. alijibu baba kisha akaniuliza..""vipi chuo unaenda lini.. kesho baba... lakini sasa hivi ahueni kidogo maana kipindi kile tulikua tunakaa mbali... sasa hivi hata hapa nyumbani unaweza ukalala na kwenda chuo tukaziepuka gharama za bweni au unasemaje SAM...?? ""Maneno yale aliongea baba kuhusu mimi kua nalala nyumbani maana nyumba yetu tuliojenga ilikua karibu na chuo.. tofauti na mwanzo... tulikula chakula cha usiku pamoja.. na ilinipasa niende nikalale niliogopa sana kuingia chumbani kwangu maana muda wote niliwaza juu ya TUNU.....
nilipopiga hatua kuingia ndani..sikuamini...nilikuta hali imebadilika katika chumba changu... kilikua chumba cha kupendeza... na kitanda kilikua kimebadilika... hakikua kitanda changu cha kawaida... pembeni kulikua na kijimeza kidogo cha ranhi ya dhahabu kilichokua kina mishumaa mi nne ikiwa inawaka... nilistaajabu na hogu ikiwa inanidunda... niliangalia mlango sikuuona... nilihisi kama niliokosea mlango mbona chumba hichi kilikua kikubwa... ghafla nilipoangalia mbele... macho yalifunguka zaidi... niliona kuna mlango...uliookua umefunguliwa nikasogea na kuona maua mengi sana na vinywaji vikiwa katika sehemu zake... nilijiuliza je niliingia mlango wa chumba changu au waapi.... roho ikanipasuka baada ya kuona...

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA