JINI TUNU... SESON 5

""Maneno ya bibi.. yalinishangaza sana.. hasa baada ya kuniambia mzimu wa TUNU ulisumbua na uliua watu wengi sana.. katika maeneo yale.... hasa wanakijiji walotumia pale kama sehemu ya mazindiko.... na je kwanini... Jini TUNU aliniandama mimi.. ?? nilibaki na siri rohoni...
Nilibeba mizigo yangu na kwenda kituoni nikisaidiwa na mtoto wa jirani maana mizigo ilikua ni mingi sana...

...
..
Nipo ndani ya gari.. miti ikirudi nyuma huku zikiwa ni hatua na dalili za kuacha kijiji pendwa alichoishi bibi...na walipozaliwa baba zangu...
....palipojaliwa neema ya mazao.. na mifugo ya kutosha..udongo wenye rutuba.
gari lina yoyoma kuzikata mbuga huku harufu ya mjini nikiisikia... barabara chakavu zisizo angaliwa na serikali.. kiasi kwamba matairi yanapita katika mabonde huku yakitingisha mizigo iliokua juu ya gari..na kutinhisha matumbo yetu na kuvuruga bilivyomo...watoyo wakitapika..na wasiojiweza...kuku alionipa bibi anatoa milio ya uoga akijua sasa anaingia mjini...
. bibi alinipa kuku.. nimfuge mjini ili iwe ishara ya kumkumbuka....niwapo mjini...nami nilipenda sana kufuga...
...
.... Kelele za soko la KOJANI.lililopo karibia na stendi ndogo..ya pembezoni mwa mji.zinanishtua kutoka katika usingizi mzito ambao sijui ulinikamatia wapi..
na kumionesha ishara sasa nakaribia kufika.. Mjini nyumbani kwetu..
mji huu ulikua ni mji wenye watu wengi sana ..nikihisabu lisaa limoja sasa karibia kufika kituo kikubwa cha mabasi Nyumbani kwetu....
..
..
Kelele za abiria kukunja kunja mizigo yao katika siti walizo kaa zinanishtua na kunipa ishara sasaa tumefika.. wapiga debe walishika nafasi zao kujenga kelele zilizoonekana kama wimbo huku zikichanganyikana na kelele za wauza matunda nyanya..biskuti..juisi nk...waliokuja madirishani huku makuli nao wakichukua fursa zao kujinadi kutaka kubeba mizigo kwa ujira...
Hao ndio niliowaangalia maana.. mizigo niliokua nayo ilihitaji mbebaji kwa hali yeyote kwakua hapakua na umbali.mkubwa sana... na nyumbani nilipoishi..
..
..
Mapatano yalifikiana mimi na kuli mbeba mizigo kwa toroli dogo..na nilikua nyuma yeye akiongoza maana nyumba yetu ilikua karibia na shule ya watoto iliokua maarufu sana.mjini. nilichoka sana huku koo likinikauka.. milinunua maji nikawa na yanywa huku najongea.. huku kuku alionipa bibi nikiwa nimemshika mwenyewe kuhofia asije kupeperuka... na safari hii alitulia kimya...kwani alikua ameshafika mjini hivyo miti na nyasi huku hazikuepo nahisi alishangaa kuona magari na kelele kutoka kwa wasakatonge ...wa kila siku waliozitafuta riziki...mjini huku
...
..
..
Napokelewa na IRENE.. mdogo  wangu wa pekee aliojua leo ilikua ndio ujio wangu..alinisubiri kwa hamu.. nami nilimjulia maana nilikwisha muandalia matunda ya zabibu na korosho nilizonunua njiani kwaajili yake.. alipenda sana mifugo na alinipokea kuku yule na kumuingiza ndani huku akimchezea.....
Nilimlipa mbeba mizigo nikaagana nae..muda huu mama alikua hayupo.. kwani alikua akifundisha katika shule ya Msingi ya serikali hapa hapa mjini.... baba yeye alikua ni mkandarasi wa  ujenzi mjini...
Hivyo mida yao ilikua bado sana...
IRENE aliporudi shule alikaa nyumbani na dada wa kazi... pekee.. IRENE alikua mtukutu sana ,alimchezea kuku yule hadi akamfungua... nilanza kupata kibarua cha kumkimbiza ili nimfunge vizuri na nimuweke katika banda... nilimkamata na moja kwa moja nikampeleka katika banda lililokua halina.kuku kwa sasa... nilipomueka kule mara..nilisikia sauti za ajabu wakati nikikomea mlango wa kibanda..""usinifungie SAM"" sauti ile ilitoka bandani...nilipomrusha kuku yule... niliondoka pale haraka na kwenda ndani kusikia kama ilitokea ndani....nikarudi tena bandani huku nikiwa na wasi wasi nikitegesha sikio kwa makini ..huku ninae muita RENE... mara nasikia tena ::""SAM mbona wanifungia ndani"??"
Nilipiga kelele baada ya kushuhudia sauti.ikitoka bandani na yule kuku sikumuona bali nilimuona TUNU...akiwa amekaaa aliejitandaza na gauni lake leupe kubwa kama la bibi harusi...kule bandani
.. hofu na woga ukanipata...nikakimbia hadi ndani chumbani kwangu na kujifungia..nikihema haraka haraka....
....
....
...
Nini kiyaendelea..... ni JINI TUNU

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA