B.O.B WAONYESHA MFANO WA KUIGWA

Kundi la sanaa la Muziki wa BONGO FLAVER linalofahamika kwa jina la B.O.B the Dreamers.. maskani yao inayopatikana Mkoani KILIMANJARO katika kata ya KALOLENI..
KATA yenye utajiri kutokana na rasilimali zake.. kama chemi chemi na uoto hai wa asili kama misitu....

KATA ambayo iliaminika kua na eneo lenye viwanda vingi kuliko mkoa wowote Tanzania...ila sasa vimekufa kutokana na kile kinachoitwa uzeefu wa umakini katika vichwa vya viongozi wetu.. hali ambayo...imepelekea viwanda hivyo...kufungwa na kutofanya kazi tena.... ikiwa lipo jopo la wawekezaji...kedekede wakitafuta fursa za uwekezaji....ila viongozi wameshindwa hilo
Kutokana na KATA ya KALOLENI kusadikiwa kulibeba jina la Mkoa wa Kilimanjaro hasa kwa muonekano wake kutokana na chem chem za njoro zinazoaminika zinatirirsha maji yake kwaajili ya chanzo cha miamba ya mitirirko ya chem chem za mlima Kilimanjaro.... Kata hiyo yenye vyanzo vya maji takribani  7 hadi 10 imetakiwa iwe katika hali ya usafi sana ki mazingira kwa ujumla....kutokana na kuvilinda vyanzo hivyo kipindi cha kiangazi....

Serikali y ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi  imekua ikisisitiza hali ya usafi bila kufutilia mkazo hivyo kuoelekea sehemu mbali mbali kua katika hali ya uchafu na mazingira kuharibika....
Kutokana na hayo yote kundi la sanaa B.O.B The Dreamers.. wameamua kuanzisha kampeni inayoitwa B.O.B THE PMT (Postive Movement Team) ikiwa kengo lao ni kuleta mabadiliko Chanya kwa njia ya kujitolea......
Hivi karibuni B.O.B walidhihirisha hilo baada ya kuonyesha mfano wa lengo hilo kujitolea katika kuweka kata katika hali ya usafi.... huku wakitoa ujumbe kua ni muhimu vijana kujitolea hasa katika maswala ya kuweka mazingira katika hali ya usafi.. na hii itakua chachu ya kuleta mabadiliko katika swala zima la usafi ikiwa ni kulinda vyanzo vya maji na uoto ambao ni uhai wetu......
Akiongea na blog hii  bwana MOHAMED maarufu kama MELLO mmoja kati ya msanii anae unda Group la   B.O.B the Dreamers   ""alisema imekua ni muda sasa wa vijana kuamka na tukaionyesha serikali mfano hasa baada ya serikali kujisahau kidogo katika majukumu madogomadogo ikiwemo utunzaji mazingira hivyo sisi kama B.O.B tumeamua kushirikiana na vijana wenzetu katika kampeni hii ambayo itapanua fursa kadhaa na mipango kadhaa ikiwa leo tunaanzia na kujitolea katika kuweka mazingira safi ya mitaani basi siku nyingine tutajitolea katika swala lingine ikiwa hata na lengo la kua na ofisi ya vijana wa kujitolea ili kurahisisha mambo yetu sisi wana kata wa Kaloleni....kwani kumekua na changamoto kibao kwa sisi vijana...  wazee wamekua wakijisahau hasa wakiangalia siasa pekee ila sio maendeleo...ila sisi kama B.O.B  Tutajitahidi kuweka hili kua la kuigwa hata na kata nyingine... ""alimaliza MELLO...
Blog hii ilimtafuta mmoja kati ya wananchi walioshuhudia swala hili kwa  jina moja tu SELE... nae alikua na yake ya kuongea ""tunashukuru sana kwa vijana kama hawa kuweza kujitolea kabisa katika maswala kama haya maana vijana wa maeneo mbali mbali sijawahi kuona wakifanya kama walivyofanya hawa ni mfano wa kuigwa kuliko kufikiria mambo yasio ya msingi vijiweni bora wakafanya maswala kama haya ya kujitolea kwa pamoja kwasababu ndio kata yao hawawezi kuiacha ikawa kata mbaya nawapongeza sana...""

..........

Blog hii inapenda kuwapongeza wana B.O.B THE DREAMERS kwa kampeni yao ya PMT kwani wasife moyo kwani wameanza vizuri.. na huo ndio mwanzo mzuri..

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA