NISHA AFANYA MAAJABU
Msanii wa Bongo muvie mkali wa uhusika.. anaebadilika kama kinyonga hasa katika uchezaji wake ... ambae anatendea haki katika nyanja za uchekeshaji... pia.. SALMA JABU (NISHA) anaetambulika kwa jina la NISHABEBEE.... aandika historia mpya baada ya kutenda maajabu katika swala zima la mauzo katika filum yake mpya ya MTAA KWA MTAA... msanii huyo alikiri hilo kutokana na filum hiyo kupokelewa na mashabiki wengi katika soko la mauzo na kufanya vizuri..
""Akiongea na blog hii meneja wa NISHA FILM PRODUCTION bw OTHUMAN (OCHU) ""alisema kua filum hii imepokewa vizuri sana na mashabiki wamesifia kazi hio iliofanyika kwa ustadi zaidi...
..""blog ilimtafuta mmoja kati ya mashabiki wa NISHA alietambulika kwa jina la DOREEN Mmiliki wa (REENS PUB) aliobahatika kuiangalia filum ya MTAA KWA MTAA alisema ""kusema ukweli filum ya MTAA KWA MTAA imenifurahisha na ujue NISHA hakoseagi ametufunza na ametufurahisha sichoki kuiangalia yaani kwa siku lazima niitizame..""
""Filum hiyo ambayo inamaliza wiki moja sokoni lakini inaonekana kama imetoka jana tu kwani kila mmoja amekua akiikimbilia kopi yake halisi na kukaa nayo ndani.. "" NISHA akinukuliwa akisema kua alichokifanya ni kizuri na ukitaka uamini kama hujaitizama nenda kaipate NAKALA yako HALISI ya MTAA KWA MTAA...
Ata hivyo kuna wasi wasi na fununu kua Filum hiyo ndio iliofanya mauzo makubwa san katika filum zote zilizosimamiwa na STEP INTERTAINMENT...toka kuanza kwa mwaka huu... blog ikipata ukweli wa hilo itatanabaisha..
Comments
Post a Comment