NISHA AWAPA MATUMAINI WATOTO YATIMA

Msanii SALMA JABU (NISHA)
Nyota wa tasnia ya filam za maigizo Tanzania maarufu kama (Bongo Muvie) hapa nchini Tanzani na msanii aliewahi kupata Tuzo za msanii bora wa kike wa vichekesho mwaka  2013-2014... na ni msanii wa pekee aliobahatika kua na vipaji lukuki katika Tasnia hiyo....

...

..
""Blog hii ilishuhudia Tukio la aina yake lililofanyika tarehe 20 /06/2015 ambapo msanii huyu alitumia fursa ya umaarufu wake kufanya kazi za kijamii ikiwa ni kuwakumbuka watoto wanaoishi katika vituo vya malezi kwa watoto waliokua wanaishi.katika mazingira magumu na  hatarishi na watoto waliokua yatima..... (waliokosa malezi baada ya pande moja ama zote za wazazi kufariki)

...
..Mbali na NISHA kufanya kazi za sanaa na kumfanya kujulikana Tanzania nzima kwa kazi zake nzuri...pia NISHA alitumia fursa hiyo kuweza kuonyesha moyo wake ikiwa ni kama mfano wa vitendo na kutoa munkari kwa wasanii wenzake... kwa kitendo cha kukaa karibu na watoto hao wa kituo cha NEW HOPE GROUP  (kituo cha kulelea watoto waliokua wakiishi katika mazingira magumu/hatarishi na YATIMA) .NISHA alitumia muda huo...kucheza nao kufutari pamoja  kubadilishana mawazo ..Kula pamoja..na kuwasaidia kwa kile kidogo alichojaliwa.....
..Blog hii ilikua na maswali machache ya kumuuliza SALMA JABU (NISHA) Juu ya uwepo wake katika tukio ambalo ni zaidi ya zawadi ya Matumaini kwa watoto hawa..wa Kituo cha NEW HOPE GROUP.. kiliopo MWASONGA... mtaa wa SHARIFU... katika Kata ya KISARAWE...

BLOGER: (sweetstoryz)""ni changamoto gani wanazo kutana nazo zinazo wakabili watoto wanaoishi...katika vituo kama NEW HOPE..hadi kukupelekea ukajitokeza mara kwa mara...katika vituo hivi..?

NISHA:Changamoto wanazokutana nazo ni  shida mazingira wanayoishi yanakua hayatoshelezi  kwani watoto hawa wanahitaji support yetu tuliojaaliwa uwe msanii ama la.. kama Mwenyezi 'Mungu kakupa uwezo kidogo hauna budi kugawana na wenzetu..hawa 
Pia wanahitaji mapenzi hata usipowapelekea kitu kwa kuwatembelea na kuwaonesha mapenzi nao wanafarijika sana
Ukichukulia mfano nilipokua katika kituo cha NEW HOPE....kuna mtoto mdogo apatae miaka minne alininong'oneza na kuniambia ""mama nibebe.. nikambeba akanilalia mabegani, kiukweli nlijifunza kua upendo na upweke ni kitu ambacho watoto hawa wanahitaji..hasa wanatamani nao kua karibu na wazazi...hivyo ukiwa nao nao wanajisikia..kua ni miogoni wa watoto walio na wazazi.

BLOGER(sweetstoryz):Ni mahitaji gani muhimu ambayo kwao pia imekua ni changamoto na wanahitaji......si kwa wao tu hata vituo vingine..?

NISHA:: "" Kiukweli watoto walio katika vituo wanakabiliwa na ukosefu wa vitu vingi ambavyo ni...muhimu kwani ni vitu ambavyo vinaisha wakivitumia hivyo wakivipata inakua ni ahueni kwao...Mahitaji muhimu kama
..chakula, mashuka,sabuni,maji safi..na kuboreshewa zaidi nyumba zao.. .....
Hata pia swala kuu la umuhimu ni ELIMU wanahitaji kusapotiwa sana kuhusu Elimu ya watoto hawa.

BLOGER:(sweetstoryz):je SERIKALI inamchango gani juu ya kundi la watoto wanaoishi katika vituo na wale wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi.. kwa jinsi..ulivyoona...?

NISHA::Serikali kama serikali siwezi izuungumzia sana kwenye mchango,kikubwa naomba niwaombe nguvu zao na kuomba wadau na wadhamini.. wasaidie watoto hawa na familia zisizojiweza na kuwatia katika bajeti ili kupunguza idadi kubwa ya jamii hii inayoongezeka kwa kasi pia serikali itambue kua jamii ya watu wasiojiweza ndio inasababisha ongezeko la watoto wengi mitaani....
Pia nawashauri watu maarufu...wenye uwezo wawe na moyo wa kusaidia watoto hawa kwani dua zao zitawaletea matunda mema,kuliko kupoteza mamilion yasiyoweza kuja kututetea mbele ya yaumulkiyama

BLOGER(sweetstoryz):Kipi kifanyike kwa jamii ya watoto hawa waishio katika vituo na wale ambao hawajabahatika kuwepo ndani ya vituo....?

NISHA::"Nnachopenda kifanyike tuzidi kujitokeza kuwasaidia haswa wenye uhitaji,tusifanye kwa fashion tufanye kwa ajili ya Allah Subhannahu WataAlla..na serikali ijaribu kuwasaidia wanaojitokeza kuwakusanya watoto hawa na kuwaweka katika kituo... kuwasaidia kukabiliana na changamoto kama MALAZI..ubora wa Nyumba..na sehemu za kulala..kukabiliana na Maradhi...kudhibiti Afya zao ziwe njema..

.....

Blog inaomba ""Wizara ya jamii jinsia na watoto.. inaombwa kuwaangalia kwa jicho pevu jamii ya watoto wa mitaani ambao inazidi kuongezeka kila kukicha, kwani vituo vimekua havikidhi idadi ya watoto hao nchini ambao ni wengi sana....






TEAM NISHA walioongozana na NISHA katika kuwatembelea watoto wa NEW HOPE

Team NISHA wakimuunga mkono NISHA walipotembelea kituo hicho... cha NEW HOPE

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA