DU! ALLYKIBA HII NI ZAIDI YA SIRI....DAVIDO ATUMBUA JIPU..R KELLY.... CHRISS BROWN WATAJWA....

Ally S Kiba  (Ally Kiba) msanii wa Tanzania  nguli na nyota wa mziki wa Bongo flaver... mmiliki wa Tuzo 5 ZA kili Music award 2015...
Hivi majuzi imesemekana mkali huyo wa Bongo Amekua akifanya mambo yake kwa siri bila kujionyesha na hii ndio inayomfanya Nguli huyo azidi kua gumzo na kuzidi kung'ara katika Soko japo ni wakitambo kidogo..
Hapa nchini wasanii wengi wamekua wakishindwa kudumu katika umaarufu kutokana na kile kinachodaiwa kufanya mambo yao kwa pupa na bila mpangilio.. ila kwa Allikiba imekua ni Tofauti..

DAVIDO ATUMBUA
Msanii mkali wa miondoko ya Skeleu huko nchini Nigeria na mtetezi wa tuzo ya Msanii bora wa kiume katika Tuzo za MTVMAMA za mwaka 2015.. msanii Davido ..Alitumbua jipu (siri) ambayo haikuwahi kusikika... iliohusiana na kutoa nyimbo na msanii mkubwa wa Tanzania ambae ni Allikiba  .. Davido ameshawahi kufanya ushirikiano ambao ulileta mafanikio kwa msanii wa Bongoflaver nchini Daimondplutnums ambae nae alibahatika kupata Tuzo ya msanii bora mtumbuizaji...Tuzo za MTVMAMA 2015. 

Milard Ayo akiongea na Davido katika Intervew iliofanyika katika Mchakato wa utoaji Tuzo hizo za MTVMAMA huko Afrika ya Kusini.. Davido alithibitisha kua hivi karibuni itasikika kazi mpya alioshirikiana na Msanii Allikiba..

Huku maneno yakiongelewa ya hapa na pale baada ya Davido kutanabaisha hilo.. maswali mengi yamekua yakijitokeza kua kwanini Allikiba hajawahi kudokeza hilo.. au hata kuonekana akiwa pamoja na msanii huyo.. kama wafanyavyo wasanii wengine...wanaopata fursa na kuremba page zao mitandaoni kwa mapicha.

KIMYA CHA FUMBUA MENGI

Usiri huo ambao unatiliwa wasi wasi kua pengine msanii huyo akaweza kua na kazi ambazo amefanya na wasanii wakubwa ila  amefanya siri.. ""Ujue swala la kutoa ngoma na Davido halafu ukanyamaza na kusubiria Suprise ni jambo kubwa huenda Allikiba ashatoa nyimbo na R Kelly au ChrissBrown maana ilisemekana halafu tetesi hizo zikapotea.." alisema mmoja wa mashabiki wa Allikiba..  tetesi za kufanya kazi nyingine na R Kelly zilitokana na mkali huyo wa Marekani kuwahi kufanya kazi moja ambayo ilimpa mafanikio Allikiba.. Kila mmoja yupo macho kuona kwa mara ya kwanza.. Davido akiwa katika kazi moja na ALLY KIBA..

Ally Kiba 

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA