NISHA AWAWEKA MASHABIKI NJIA PANDA YA CHINA

Msanii wa Maigizo mkali wao hapa Bongo mwanadada mahiri mwenye vipaji lukuki katika Tasnia ya BONGO MUVIE... SALMA JABU (NISHA) awaacha Watanzania na Sintofahamu ya kutoelewa nini anamaanisha....baada ya kutuma maneno Kuntu katika moja ya kurasa zake..
Msanii huyo hivi majuzi alipata shavu la aina yake baada ya kupata mwaliko mkubwa wa kwenda Ughaibuni(CHINA) kutokana na shuhuli zake za Kisanaa..
Huku safari hiyo ikiwiva.. mkali huyo wa vichekesho na tajiri wa kubadilika badilika katika kiwanda cha Bongo Muvie.. amenukuliwa akisema...
"""
・・・
Nna suprise kwenu wapenzi..ingawa suprise haisemwi ila mi nimetahadharisha tu,Tafadhali naomba muyapokee  maamuzi yangu hayo ntakayoyachukua... pls isije  kugawa  mashabiki zangu.. kikubwa sintobadilika kitu ntazidi  kuwapenda ... Safari yangu ya China ina vipengele  A na B.. hiko A ni mtihani mtupu ila mtanivumilia.. #Alamsiki... nawapenda wote..
...
...
Msanii SALMA JABU NISHA

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA