NISHA AZUA BALAA LINGINE
Mkali wa vichekesho mwanamke Bongo SALMA JABU NISHA ...na mwanamke pekee aliokua na utajiri wa vipaji lukuki... hivi karibuni azua tafrani katika mitandao ya kijamii..
TAFRANI
Mwanadada NISHA alitoa kanyaboya iliofanya watu wakambatiza majina ambayo mengine yalichekesha kwa utamkaji wake..
Mashabiki walivutana huku na huku eti kwa lengo la kumtafutia jina ambalo litamfaa .. hiyo ni baada ya kuitangaza ndoa ya yeye mwenyewe..
Mashabiki walipokea mpira huo ambao ulikua na mtihani wa kuteua jina zuri atalolipenda kwani aliahidi itampasa abadilishe jina hilo..baada ya kuitangaza ndoa yake.
ALIPATA JINA
Nisha alivurumishiwa mvua ya majina kutoka kwa mashabiki wake huku jina hilo likiwataka waendane na cheo chake alichojipachika baada ya kuolewa..
Hata hivyo kutokana na majina yote hayakuendana na nia na dhamira ya yeye kujioa alionekana kuyapishilia mbali.. huku akiendelea kubaki na jina lake linalompa ugali ....jina la NISHA BEBE...
TETESI
fununu zina dai kua mwanadada huyo yupo mbioni kuonyesha nia dhahiri iliompeleka CHINA ambapo ndipo alipo kwa sasa.... "pengine atarudi na shemeji wa kiukweli.."" ilikua ni moja ya maongezi ya mashabiki zake wakiulizana ...huku wakidhani pengine yupo mshefa wa kuvimba macho aka Mchina akiwa labda ndio shemeji yetu.
Hata hivyo taarifa kutoka chanzo cha mtu wa karibu wa mwanadada huyo jina kapuni....alikanusha na kusema msanii NISHA .. amekwenda CHina.. kwaajili ya maswala...ya sanaa ama kutokana na kufanya vizuri katika ulimwengu wake wa sanaa...
Comments
Post a Comment