HEE! NISHA ATEKWA CHINA.. AWA TISHIO

Msanii wa Maigizo na Filum za umakini na zile za kuchekesha nchini Tanzania mwanadada NISHA... (SALMA JABU)
Ambae majuma kadhaa yaliopita aliingia katika Vichwa va habari baada ya kushutumiwa na baadhi ya vyanzo vya habari kua amekwenda CHINA kwa mwenza...(MCHUCHU)


Shutuma hizo ndiyo ambazo zilimuangukia NISHA alizijibu kwa aina yake baada ya kumuonyesha mpenzi huyo ambae alimfuata huko CHINA... Ila tafsiri alioitoa NISHA ni kua hakwenda CHINA hivihivi ila amekwenda kwaajili ya SANAA ambayo ndio kazi inayomzunguka maisha yake ... na kusema katika swala la mahusiano huko CHINA atakua yeye kama yeye.. ndio hali iliopelekea mwanadada huyo kujimiliki mwenyewe katika mahusiano..

NI TISHIO
Nisha hivi juzi kati alianzisha sintofahamu katika  mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa ametokelezea... katika maeneo mbali mbali  huko nchini CHINA... mwanadada huyo alionekana mitaa mbali mbali akiongozana na wenyeji wa nchini humo huku akizua fununu kwa  raia wa nchini Tanzania ambao wanaishi huko ughaibuni..wakidhani kua mwanadada huyo huenda akawa anajifua hasa hasa katika maswala ya sanaa ambayo nchini humo yanatumia Teknolojia ya hali ya juu .pia baadhi walimsifu jinsi anavyoendana sawa na raia wa CHINA ambao wengi wao hawatambui kuongea lugha yeyote zaidi ya KICHINA.. kutokana na kipaji chake alielewana nao na walifurahia nae..muda wote huku wengine wakimtaka wapige picha za ukumbusho...

ATEKWA..
Msanii huyo Alionekana akiwa bega kwa bega na raia wa Nchini CHINA ..jambo ambalo linasadikiwa huenda NISHA akayahamishia makazi yake huko na kuendeleza sanaa katika nchi hiyo.. kutokana raia wengi wa CHINA wanaonesha mapenzi ya thati ya kumkubali NISHA  hasa kwa Kazi zake za SANAA....

Hata hivyo mwanadada huyo NISHA alizidi kusisitiza kua CHINA ni nchi ambayo amekwenda kujifunza sanaa ili aweze kubadilisha muonekano wa sanaaya Bongo iendane na Teknolojia.. hivyo ni ngumu sana mwanadada huyo kutokomea huko... kwani anaipenda Tanzania...

NISHA KATIKA UBORA WAKE

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA