JOKATE..."TUZO YA DAIMOND YAONESHA WANAFKI WANGU... BABU TALE ..DAIMOND WATAJWA
Huku hongera kama mvua zikishuka kwa mkali wa mziki Bongo Daimond Dangote.. baada ya kupata Tuzo ya MTV MAMA ...huku akishukuru Mashabiki zake kwa kuweka maneno matamu katika kurasa yake... Pongezi hizo zimekua ni za pekee baada ya kuitangaza Tanzania kwa kuipeperusha bendera ya Burudani..
Mkali huyo aliotwaa Tuzo hiyo alikua na mastaa kibao wa Afrika kama Davido Yemi na wengi.kutoka Nigeria...
DAI AMTIBUA JOKATE
mkali huyo mshindi wa tuzo ya mburudishaji bora.. amemchefua staa mwenzake JOKATE MWEGELO.. mwana mitindo huyo na mshiriki wa miss Tanzania miaka iliopita ambayo inadaiwa alishawahi kua mpenzi wa Chibu aka Dangote .. alionesha hali ya kuchukizwa baada ya Chibu kutoa kinyongo Kwa kurusha video ambayo ina muonesha JOKATE akiserebuka nyimbo ya mdogomdogo... ingawa video hiyo ni ya kitambo na haihusiani na ushindi wa Daimond.. JOKATE alitoa ya moyoni.. na kuwaorodhesha watu ambao hakudhani kama wangesapoti kile alichokifanya Daimond bila idhini ya JOKATE
UJUMBE ALIOTOA JOKATE
Tuki-support mtu ndio kama hivi matokeo yake mtu anatumia baadae kukudhalilisha. Hii video aliyo-post kwanza ni #TBT kama sijakosea mwaka jana mwishoni nilikuwa sehemu na my friends @bikira_wa_kisukuma akani-record na kumtumia @diamondplatnumz bila mimi kujua. Kiukweli sijui kwanini walifanya hivyo. Nikaja kujua baadae sana na nikaona sio big deal cause kila mtu anapenda mziki na sio dhambi kucheza mziki wowote uupendao. Ila kitendo cha @diamondplatnumz kwenda kuitafuta huko ilikokuwa hii video clip na kui-post leo najiuliza maswali mengi 1, anataka ionekana kama nilikuwa nashangilia ushindi wake? Which is not bad hakuna ubaya hapo kama unaamini ushindi wake ni sifa kwa taifa ila 2, Kwanini a-post na caption ya Na Bado Mtanyooka? Ili amkomoe nani? Au kwasababu niko karibu saaana na @alikibaofficial anatafuta kutuchonganisha? Ili iweje? Mimi I believe life goes on na kila mtu ana uhuru wa kumpenda au kuwa karibu na yule apendaye na kum-support ndio maana hata mimi nimekuacha na your new life 3, Pengine ni kweli anaendeleza zile hulka zake za kudhalilisha wanaweke aliokuwa nao waonekane sio kitu just because hawako na diamond platnumz chibu dangote. Which to me is just dead wrong. @diamondplatnumz hizi sio tabia tunazozitegemea kwa mtu anayejisema anakomboa mziki wa Tanzania sio kwa kuweka visasi na fitna zako wazi wazi hivi. Unatu fanya tukose imani nawewe zaidi na tunaogopa ku-support cause hukawi kutugeuka. Kuwa tofauti basi, onyesha mfano kwamba kweli hupendi beef unapenda mziki wa Tanzania uendelee ila kwa ulichoki-post unaonyesha wazi UNA visirani na hutaki mema unatafuta drama, kiki, vurugu unataka kila siku uwe wewe tu ambazo kiukweli mimi binafsi siziwezi utaendelea kushinda wewe tu katika hilo na sitashindana nawewe katika hilo kwasababu siwezi nawewe unajua kama ulivyoniimba mimi mpole, sinaga maneno ( ila kwenye kazi ndio nakuwa mkali kama pilipili ). Ila ungetumia busara kidogo. Just move ON kiroho safi. Naomba pia nitumie fursa hii kukupongeza kwa tuzo yako ya MTV ila @babutale hata wewe ndugu yangu? Is this how tunaendeleza so called uzalendo? Inshallah Kheri lakini yote maisha wanyonge sisi iko siku Mungu atatunyanyua.
Comments
Post a Comment