HAPPY : NIKIPATA MDHAMINI SIFANYI MAKOSA

Msanii Chipukizi wa Bongo flaver.. HAPPY SULEIMAN.. (HAPPY) anaefanya vizuri sana katika  kuja juu katika kinara hichi cha wanawake wachache wanaokuja juu katika kiwanda cha kupeperusha bendera ya muziki wa kizazi kipya...
 
Ambae aliwahi kutamba na kibao cha Nakupenda ...ambacho kilishika chati sana kibao hicho kilipikwa vizuri na kupendwa na watu kedekede...
Katika kutafuta soko la kutangaza kipaji chake ..wimbo wa Nakupenda uliingia katika mtafaruku ambao (HAPPY) alisema asingependa kuelezea  nini kilitokea.....
   Ila katika chunguza za blog hii iligundua kua nyimbo hiyo iligongana idea na msanii wa kike (jina kapuni) nae chipukizi na kufanya nyimbo hiyo kuonekana ni kama imerudiwa mara mbili..
  Swala ambalo (HAPPY) alipiga moyo konde na kusamehe hata gharama ambazo zilimgharimu katika kuitayarisha ngoma hiyo ..kwakua ngoma hiyo ilishatambulika ilimpasa aisimamishe kutokupigwa katika media ili kutoa utata....
       "kutokana na nguvu nyingi kumalizia katika ngoma ya kwanza hususani katika maswala ya mtonyo (pesa)... (HAPPY) alishindwa kupata udhamini wa kumpeleka studio kwa kipindi hicho ingawa  alijiamini kwamba sanaa kwake haiishi na ni kipaji chake... aliomba kama kuna alietayari kumsaidia basi yupo tayari kuingia mikataba ya aina yeyote inayohusiana na mziki kwani anajiamini hakuna wakumshinda Tanzania (kujiamini ndo mpango)
.....  hivi majuzi (HAPPY) alitumbuiza katika birthday ya msanii wa Filum Bongo Nishabebe ambapo alionyesha kipaji cha masauti na kuacha kila muhudhuriaji kinywa wazi huku wengine wakimfananisha
na Rubby...kwa sauti yake kali nzurii..

HAPPY.. alielezea ndoto zake za kufanya kazi na wasanii wajuu akiwemo Barnaba kwani anahisi watalandana na watafanya jambo kubwa....


Kama una Malengwa na kumsaidia HAPPY au kupata kazi aliofanya...au kutaka mawasiliano..pitia wasap number +255656278685

...........HAPPY katika ubora wake

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA