NISHA AKOSA DHAMANA CHINA... AFUNGUKA AKIWA KIFUNGONI
Msanii mchekeshaji wa kike wa TANZANIA...
Na muigizaji wa kutamba katika Tasnia ya BONGO MUVIE .. SALMA JABU NISHA..
Hivi majuzi akiingia katika habari ya sintofahamu ya kukamatwa na mihadarati..huko nchini CHINA alipotia kambi toka jully...katika moja ya shughuli zake za sanaa.
MASHABIKI WATOKA MACHOZI
Habari hii ya kukamatwa na madawa ya kulevya ilikonga nyoyo za watu na kwa maumivu kabisa baada ya mashabiki zake kutokuelewa ukweli wa chanzo hicho kilichosambaa bila ukweli kufahamika..kua ni kweli na nini hatima yake
AKOSA DHAMANA
Huku mashabiki wakisubiria dhamana ama tamko la hukumu kutoka kwa NISHA mwenyewe ama serikali ya CHINA ama wenyeji wake.. bila mafanikio... kwani hakuna aliojitokeza kulizungumzia hilo hata ikiwemo serikali ya Tanzania... moja kwa moja ilionekana hakuna ukweli ndani yake wa jambo hilo..
Tulizoe kuona watanzania wengi wakihukumiwa na kuzungumziwa ila kwa NISHA hakutokea mtu yeyote..wa serikalini au binafsi..kuongelea asilimia 100 hakukua na ukweli ndio maana hakutokea mtanzania yeyote kusema anafuatilia ili atoe dhamana...kwa msanii wetu..huko CHINA kama atakua yupo kizuizini
NISHA AFUNGUKA
Kwa mara ya kwanza NISHA awadhihirishia MASHABIKI kua hakua katika kifungo wala kushikwa na mihadarati kwani yeye hakuenda kwa kazi hiyo.. ila ni.kawaida wageni wengi wakiingia CHINA ama nchi yeyote kukaguliwa ni muhimu na ndicho kilicho fanyika yeye kama mgeni...
""Historia ya Watanzania wengi hasa wasanii waingiapo CHINA husachiwa sana kutokana na kumekua na matukio mengi sana ambayo yanahusishwa na ukamatwaji wa madawa kwa raia wa TANZANIA wanapokua wanaingia ama kutoka nchini humo.. hivyo serikali ya CHINA imekua makini sana kwani sio sheria kuvusha madawa ya kulevya kwa nchi ya aina yeyote duniani... kwani hakuna nchi ambayo inakubali kua Mlango wa kuingiza ama kupitisha madawa ya kulevya... alisema NISHA katika moja ya kurasa zake mitandaoni...""
Huku akitania kua Ataozea jela.. na wakazi wengi wa huko wakiita CHINA kua ni lupango JELA kwa ufuatiliaji...wa MIHADARATI.
Comments
Post a Comment