WEMA: MIMI NI CCM DAMU GOLI LA MKONO LAZIMA...MSIOJITAMBUA NENDENI UKAWA
Mwanachama halali kabisa wa Chama Cha Mapinduzi CCM .. dada mh Wema Abraham Sepetu.. ambae pia ni msanii wa sanaa Tanzania pia unapotaja watu maarufu AFTICA MASHARIKI basi huachi kumtaja WEMA SEPETU..
Mlimbwende huyo ambae ni mstaafu wa Taji la Miss Tanzania miaka ya nyuma...
katika mbio za uchaguzi 2015 aliingia katika kinyang'anyiro cha ugombeaji wa kiti maalumu ubunge CCM huko SINGIDA ambapo katika michakato wa upigaji kura.. hakubahatika kunyakua kura nyingi ambazo zingemuwezesha kupewa kiti maalum cha ubunge....
...
..
Huku kukiwa kuna fukuto la kura za maoni za uraisi yalitokea mambo mengi ikiwa ni baada ya MH Edward Lowasa Kukatwa katika majina pendekezwa mbali na kupendwa na watu wengi ilipelekea watu wengi kumfuata LOWASA alipo hamia chama pinzani cha Chadema ambacho kinaongoza Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA ... moja ya watu walionyesha nia thabiti ya kuhama katika chama cha CCM ni wasanii lukuki ambao walitangaza wazi...
WEMA SEPETU AWAPA YAO
baada ya kuonekana wasanii wengi wamesaliti chama na kutoonesha uzalendo .. wengi walizusha na kudai kua WEMA nae ameingia katika chama cha CHADEMA swala ambalo alilikana na kuwaonya Team wake (TEAM WEMA) wanaotumia jina lake kuwapigia kampeni UKAWA kua waavhe mara moja au wajivue jina lake.. kwani yeye hawezi kuhama wala kuondoka CCM...
Na aliwaambia wanaohama hawajitambui na kujielewa
WEMA APATA SHAVU IKULU
huku msanii WEMA bila kufa moyo aliedelea kunadi chama chake bila kujali kama hakuipata nafasi.... aliendelea kumnadi mgombea teule wa uraisi Bw John Pombe Magufuli...
Pia alionekana katika viwanja vya ikulu akiwa ameambatana na wasanii wenzake akiwemo Steve nyerere ambae nae aliwania uteuzi wa ubunge...... wasanii hao walionekana kupata shavu kwa raisi JK baada ya kuonekana kwa ukaribu kabisa.
Minong'ono inasema huwenda wasanii hao akiwemo WEMA wakawa wamepewa kazi ya kuwa bega kwa bega na Magufuli.. katika mbio za kampeni.
GOLI LA MKONO
Msemo huu umekua chachu sana Kwa CCM katika mbio za kampeni hizi kwani CCM kupitia NAPE wamesema kuwepo kwa wasanii itakua chachu sana ya watu kujitokeza katika mikutano ya kampeni..hivyo ushindi utakua kama kumsukuma mlevi...
Huku wakisema USHINDI NI LAZIMA.
Comments
Post a Comment