NISHA KUNUKIA CCM.... MAKADA WAPANDA DAU

Msanii wa Filum za Kibongo nchini SALMA JABU NISHA... anaesifika kwa kua ni moja kati ya wanawake wachache Hapa nchini ....kwa kujituma na kua wabunifu hasa wanapoonekana wakipambana wakitumia vipaji vyao kuinua maisha yao...

Katika kipindi hichi cha kampeni na mbio za kukimbilia Uchaguzi mkuu wa maraisi ..madiwani na wabunge kumetokea  nenda rudi ya wasanii kujigawa kwasababu ya itikadi ya vyama huku kupelekea wasanii hao kunadi vyama ambavyo walijihusisha navyo....

WASANII WAJIGAWA.
wakati kampeni zikizidi kuchanja mbuga huku kila chama kikinadi sera zake ... ilikua hivyo hivyo katika makundi ya wasanii waliopo katika vyama hivyo..
Vyama vikuu ambavyo vimo katika ushindani mkubwa ni CCM na vyama vilivyo unda umoja almaarufu UKAWA..
Wakati CCM ikimnadi mgombea wake wa Uraisi kupitia tiketi ya chama hicho DK JOHN POMBE MAGUFULI... Huku UKAWA wakimnadi mgombea uraisi.kupitia chama hicho MH EDWARD NGOYAI LOWASA.
moto huo ulikolezwa na makundi ya wasanii ambayo yanasindikiza kampeni hizo pande zote mbili.. wasanii wengi wamekua wakirushiana vijembe katika mitandao ilimradi kila mmoja anajinadi...

FUKUFUKU
penye moshi kuna moto.. baadhi ya wasanii wachache walihama katika chama cha UKAWA na kuhamia CCM wasanii hao ni Chuchu hans...Ray..Aunty Ezekiel...
Wasanii hawa wanadaiwa kununuliwa .. tetesi ambazo walizikataa kupitia vyombo vya habari...ila walidai wamefuata sera...

NISHA MBIONI..

Huku idadi ndogo ya baadhi ya wasanii ambo hawajaonesha uwepo wao wa chama chochote katika kipindi hichi.
   swala ambalo limetafsiriwa kua ni uamuzi wa busara..  kwani muda wa kampeni wasanii wengi wamekua wakiishi kwa uhasama  na kupigana vijembe huku wakisahau kua yapo maisha baada ya uchaguzi...

Hali hiyo inawafanya baadhi ya wasanii kutokuonyesha wao ni mashabiki wa Chama gani wala kufungana na upande wowote baadhi ya wasanii hao ni SALMA JABU NISHA nae ni mmoja wapo...

MAKADA WAPANDA DAU 
Inasemekana wasanii ambao hawatambuliki wapo chama gani wamekua wakitafutwa na Vyama hivyo  kwa gharama zozote ili wapate kuwavunja nguvu wapinzani wa kila upande...

....
Hali ya sintofahamu ilikuja pale NISHA alipoonekana amevaa nguo yenye nakshi na rangi zinazoshabihiana na rangi za bendera ya CCM ila msanii NISHA aliweka wazi kua nguo aliovaa haimaanishi kua yeye ni mshabiki wa chama husika.. ila siri yake iko moyoni...
""Au amenunuliwaaa,,?"
Ni baadhi ya maswali ambayo mashabiki zake walikua wanajiuliza katika moja ya kurasa zake mitandaoni... ila NISHA alieleza kua yeye ni TEAM NO CHAMA.

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA