NISHA,BARAKA DE'PRINCE WABAMBWA LIIIVE ,NISHA AIKIMBIA AIBU AJIFICHIA CHINA (MAMBO HADHARANI)

Msanii SALMA JABU (nisha) wa Bongo Muvie ambae sasa yupo katika chart za wasanii wa kike wanaofanya kazi nzuri katika Tasnia ya Filamu TANZANIA.... Hivi karibuni ameingia  katika sintofahamu na minong'ono dhidi yake yeye na Msanii wa Tuzo ya Msanii Bora anechipukia (KTMA) BARAKA DE PRINCE ..
...
MAMBO HADHARANI
lisemwalo lipo kama halipo basi lipo njiani tena karibu sana.. kutokana na siri kua sio siri wasanii hawa waliona waweke mambo hadharani baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuwaambia watu au watu kutofahamu... Wasanii hawa walionekana kukubaliana sana na kusifiana hadharani swala ambalo sio la kawaida kwa wasanii wetu...
Matukio haya hua yanajirudia miongoni mwa wasanii kadhaa husifiana mwisho wasiku hufanya kweli (NEY na SHAMSA)... walionekana wakitupiana katika kurasa zao na sifa kedekede kati yao mwishoniiii...??
..
..
MINONG'ONO
Upele umewapata wakunaji... wale wakali wa kufuatilia SKENDO jijini walifungua masikio na macho kufuatilia baadhi ya maneno yanayotamkwa dhidi yao.... kurasa maarufu zilizofuatilia swala hilo katika mtandao wa picha na matukio wa INSTAGRAM.. na kurasa pendwa sana Tanzania hasa kunapotomea SKENDO ...kama (usipojipangantakupanga.....) (gossipe magazine) (MALKIA wa insta) nk 
waliweka bayana matupio hayo yaliofanywa na wasanii hao swala lililo onekana na wadau wanaowafuatilia kua huwenda wakawa na mahusiano....

..
.
MSHTUKO
kila mmoja anajua nini maana ya mtandao wa kijamii.. wasanii wengine hutumia kufikisha ujumbe wao kwa hadhira zao... SALMA JABU alizidi kuweka wazi huku kuwapa mia kwa mia wale waliokua hawaamini baada ya kuweka picha katika mtandao wake wa wassap na kuweka maneno ambayo yalidhihirisha kua BARAKA ana miliki mzigo....

..
..
WASEMAVYO WADAU
""Hawa wanazuiana bwana wasituzingue" ni baadhi ya maneno ya wadau waliokua wakizungumzia habari hizo mitandaoni huku wengine wakimwaga sifa kua wawili hao wanaendana....wasiachane.

NISHA AKIMBIA

Japoa waandishi walitaka habari kamili kutoka kwa wawili hao wenyewe ilikua ni tofauti.. camera za kidigitali zilitegwa maeneo ya Club 71 usiku wa tarehe 27 septemba... ambapo kulikua na shoo iliokua ikimuhusu BARAKA na wasanii wengine pia NISHA ilisemekana angekuepo kumpa sapoti mwenza wake... 

ili kupata uhakika waandishi walitia kambi bila mafanikio kwani ... NISHA aliingia mitini na hakuonekana... Habari zilizopatikana kutoka kwa mashabiki wake wa karibu zilisema kua  NISHA hayupo nchini ila yuko ughaibuni CHINA ..... taarifa za kua alikwenda kufanyaje hazikupatikana maana NISHA amekua akipageuza CHINA kama kibaha.... (safari za kila siku). Kwa upande wa BARAKA hakubahatika kuzungumzia lolote.. huku habari zikibaki kua wawili hao ni Wapenzi.

NISHA na BARAKA katika ubora wao

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA