YONDANI ANENA ASEMA KIIZA WAO HUKO HUKO
Ni vita ya soka kati ya watani wa jadi wa Tanzania Simba itakayokuwa mwenyeji dhidi ya dar es salaam yanga Africa siku ya jumamosi katika uwanja wa taifa tayari simba ipo mjini unguja katika kujiwinda na mechi hiyo inayotazamiwa kuwa Kali kwa pande zote mbili kwa upande wa yanga beki wake Kelvin yondani amesema siku hiyo atahakikisha mkali wa mabao kwa sasa katika ligi ya vpl Hamis kiiza haisumbui kabisa ngome yake ya ulinzi yanga inajivunia beki yake hasa ya kati kwa kucheza kwa muda mrefu na maelewano mazuri huku simba nayo ikijivunia safu yake maridadi ya ufungaji yanga itateremka dimbani siku ya jumamosi ikikumbuka mchezo wao wa mwisho ambapo simba ya dar es salaam iliibuka na ushindi timu zote mbili zipo visiwani huku yanga ikiifuata simba unguja ikitokea Pemba je nani ataibuka mshindi mshindi tusubiri jumamosi ya wiki hii
Comments
Post a Comment