UTABIRI WA DAIMOND HOFU YA TANDA
Huku ngoma ya Utanipenda ikiendelea kukata mbuga sehemu mbali mbali za mipaka ya nchi ya Tanzania na huku Video ya nyimbo hiyo ikiweka historia ya pekee ya kutizamwa na watu wengi sana kwa muda wa siku takribani mbili tu tokea ilipo achiwa rasmi siku ya Ijumaa..
Imekua ni kawaida msanii Daimond kuwa starehesha mashabiki zake kwa kila nyimbo mpya anayoitoa imekua ni ya tofauti na huvuta hisia za mashabiki kwa kiasi kikubwa sana.
Mkali huyo ambae ameonekana kutajwa mara kadhaa katika vinyang'anyiro vya tuzo mbali mbali nchini na nje ya Africa na amekua akileta mafanikio katika mziki wa Tanzania baada ya kunyakua Tuzo kadha wa kadha ...za kimataifa.
UTANIPENDA
Imekua ni wimbo waTaifa kila kona ya Tanzania baada ya msanii Daimond kuwaonyesha watanzania kua yeye amezaliwa na kipaji alichojaliwa na Mwenyezi Mungu...
Inasadikika kua video ya nyimbo hii hadi kufikia siku tatu itakua imevunja rekodi kubwa sana katika kutizamwa mara nyingi katika mtandao wa youtube..
Daimond ameteka hisia za mashabiki zake baada ya kuonyesha ujuzi wa hali ya juu baada ya kufikirisha kile kinacho zungumziwa mara nyingi na wapenzi wa mziki Tanzania.
Kwani tumezoea kuona wasanii wengi Tanzania huvuma mwishoni hushuka hadi maisha yao hua hayatamaniki..
Daimond amejifunza hilo hadi kupelekea kujua kua kipi kinaweza kutokea endapo hatofata misingi ya kujiongoza na kubuni njia mmbadala ya kufanikiwa na kuuacha mziki ukiwa umemueka pazuri.
TAHARUKI HOFU YATANDA
Mashabiki wamekua na maoni tofauti juu ya wimbo huu mpya unaojulikana kama Utanipenda, ambao umesambaa kila kona Nchini.
Ndani ya wimbo huo kumekua na maneno ya wazi sana tofauti na mashabiki awalivyozoea kutoka kwa Daimond,
Tukivuta kumbukumbu ya miziki ya nyuma aliowahi kuwika nayo mfano
Wa nyimbo hizo ni mdogomdogo... Nasema na wewe...nimpende nani... Nk Daimond amekua akifumba maneno sana hivyo kumfikirisha msikiizaji kwa kutafuta maana...
Ila utafouti wa nyimbo ya utanipenda.. Imekua na maneno ya wazi wazi sana na kuwafanya mashabiki wasiumize vichwa kutafuta maana,
ila moja kwa moja watajiuliza kwanini kajisemea yeye...mwenyewe...
"Huyu anajichuria marehemu Kanumba aliimba kuhusu kufa angalia baada ya siku kadhaa kilichotokea..sasa huyu nae anafata nyayo anaimba kuhusu kufikisika atafuata njia hyo hiyo atafilisika""
Alisikika akisema mmoja wa mashabiki jina kapuni..
HOFU
katika video hii Daimond amewatumia wahusika wa ukweli aliowazungumzia ndani ya nyimbo, jambo ambalo ni mara chache sana kufanywa na msanii
Yeyote
Katika nyimbo hii ni kama ameyaongelea maisha yake ya kweli ambayo pengine yanaweza kutokea..
Ila dhana hizo zimetanda katika nyoyo za mashabiki wale wanaompenda kupitiliza wakihofia pengine yanaweza kutokea hasa wakiona kuna msemo unaosema " lisemwalo lipo kama halipo linakuja"..
PONGEZI
Mashabiki wamezidi kumpongeza Daimondplutnum kwa kuonyesha uhalisia wa kile anachokiimba katika video yake hiyo,
huku wakionekana kuwatumia wahusika..watu ambao hatukudhania kama tungewaona jatika Video kama B.SANDRA (mama mzazi wa Nasibu Abdul Daimond) Babu Tale na mkubwa Fela (ma meneja wa DAIMOND)
Harmonize (msanii anaechipukia kupitia mgongo wa Daimond) Zari (mama tiffa mzazi mwenza wa Daimond)
Wote hao aliwazungumzia katika nyimbo hiyo...na wote wlionekana kutokelezea..katika video hiyo
Blog iliongea na Mshabiki damu wa Daimond BW. ABDUL alikua na haya ya kusema
"Tunaimani Daimond ni mwanamuziki ambae atakua ni watofauti hasa tukiingansha na uongozi unaomuongoza unajielewalewa kwa hiyo hatutarajii Daimond kushuka kimaisha, japo mziki anaweza kushuka kwakua hawezi kuimba maisha yake yote hivyo tunatarajia awe ni mwanga kwa wasanii wengine wanao pata mafanikio kwa ghafla... Kama Daimond..
Comments
Post a Comment