UTANIPENDA YA DAIMOND YAMUEKA PABAYA DR.MWAKA

Matokeo ya matangazo kupitia msanii maarufu Tanzania  DAIMOND yaleta tafrani kwa Daktari wa tiba asilia DR. MWAKA

Naibu waziri w Afya Muheshimiwa HAMIS KIGWANGALA siku chache baada ya uapishwaji kutumikia wizara hiyo aanza kazi na kasi ya aina yake.
Afanya ziara ya kushtukiza katika Vituo vya afya vya DR. MWAKA vinavyo julikana kama FOREPLAN CLINIC.
Vituo ambavyo vimesambaa nchi nzima.. alipotembelea eneo hilo hapo Daresalam alikuta baadhi ya wagonjwa wakiwa wametelekezwa huku wahusika na matabibu wakitembea mitini.


DR.MWAKA akiwa na DAIMOND mwanamuziki katika moja ya matangazo yaliotekelezwa na  msanii huyo ambayo yadaiwa huenda ikawa moja ta tifu tifu lililo mkumba DR.MWAKA


UTANIPENDA YAWA CHANZO

Huku mamia ya watanzania wakiwa katika adha ya kutafuta tiba ya maradhi sugu yanayo wasumbua pengine kudhani hata Hospitali haziwezi kufanya tiba, Hutafuta njia mmbadala ya kutatua matatizo hayo kupitia tiba asilia..

Huku tukisema Biashara ni Matangazo Dr .MWAKA  amejizolea umaarufu kutokana na matangazo ya biashara yake yanayoendelea nchi nzma kupitia vyombo vya habari .
Pia DR. MWAKA amekua na vipindi maalumu katika vituo mbali mbali vya TV katika kuelezea biashara yake na tiba zake ikiwa ni kutambulisha dawa zake na huduma..

Dr MWAKA amejizolea umaarufu sana hasa katika tiba za akina mama kuhusu uzazi na maradhi ya tumbo kwa kina baba na watoto pia. 
Hivi majuzi DR.MWAKA alizidi kujipa umaarufu baada ya kumtumia mwanamuziki DAIMOND katika matangazo ya biashara.
Hivyo Dr.Mwaka akizidi  nakujizolea umaarufu kwa muda mchache.
""Pengine ile video ya UTANIPENDA ni chanzo"
Walisikika wakizoza watu huku na huko baada ya kudhani kwamba tangazo lililopo mwanzo wa video ya Mwanamuziki Daimond tangazo lillokua likielezea tiba na utabibu wa DR.MWAKA
Inasemekana watanzania wengi walielekeza macho kwa Daktari huyo wa Tiba asilia baada ya wimbo ule tu kutoka.


Baadhi ya vifaa vya  utabibu vya kileo anavyotumia DR.MWAKA kinyume na sheria za utabibu.
Naibu waziri wa Afya Mh. KHAMIS KIGWANGALA.. aliofanya ziara ya kushtukiza katika vituo vya tiba asilia vya DK MWAKA.

                     



           HOFU KWA WAZIRI

huku kukiwa na rundo la madaktari wa asili wakiendeleza tiba miongoni mwa wananchi kumezuka  utapeli na udanganyifu wa kupitia mgongo wa tiba asilia.
Wananchi wengi wamekua wakilalamika kua tiba hizo hazisaidii huku wengine wakisema zina udhalilishaji wengine wkidiriki kusema ni mambo ya ajabu
"Mtu unaambiwa uweke mboga sehemu za siri ili uutibu uke si kufuru hii""
Alisema EDWIN mfanya biashara mdogomdogo wa mboga mboga kwani alisema siku za nyuma alikua na wateja wengi sana akina mama katika mboga ya aina ya mgagani, Ila aligundua kupitia mitandao kwamba kuna daktari anasema kua mgagani ni dawa kwa wanawake wenye maumbile makubwa ya siri..
Blog ilipofanya uchunguzi ikigundua kua DR.MWAKA ndio aliosema hilo katika moja ya matangazo yake hivyo kufanya rundo la akina Dada kukimbilia mboga ya majani ya mgagani inayotumiwa sana maeneo ya Tanga na kuifanya ni tiba ya tatizo hilo.
Hata hivyo Blog haikua na uhakika sana katika tiba hiyo maana haikupata mwana mama aliotoa shuhuda wa tiba ya mgagani.

Naibu waziri wa Afya HAMISI KIGWANGALA alipotembelea kituoni
hapo alisikitishwa na kitendo cha Dr MWKAA kukimbia ..hivyo alitoa maagizo kua kwa watabibu wadogo wa DR. MWAKA awasilishe vielelzo vyake katika wizara hiyo akiwa kama yeye ana uhalali wa kujiita dokta ama la...

Pia NAIBU WAZIRI amemtaka mkurugenzi msaidizi wa tiba asilia Bw POUL MOHAMED kuhakikisha uchunguzi unafanyika katika tiba ya DR MWAKA na uhalali wake wakutumia vifaa vya kisasa vinavyotakiwa kutumika hospitali.

HOFU 
huku ziara hiyo ya kushtukiza ikiendelea kumeibuka sintofahamu juu ya tiba za Daktari huyu kua huenda zikawa sio rasmi au batili..
Ila kitendo cha Dr. Mwaka kukimbia huenda ni kutokujiandaa na majibu ya maswali ambayo huenda angeulizwa...

 



TAHADHARI
Naibu waziri ametahadharisha wale wote wanaojitangaza kupitia vyombo mbali mbali vya habari kuhusu tiba ni jambo la kinyume na sheria hivyo amewataka watu wanaojiita madaktari kuacha mara moja kujitangaza katika swala la tiba zao kinyume na sheria.

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA