NISHA AMVAA ERIC OMONDI
Mkali wa filum za kuchekesha na mmiliki wa kampuni ya NISHA FILM PRODUCTION dada SALMA JABU NISHA...
anaewika na Filum mpya ya KIBOKO KABISA inayofanya vizuri sokoni toka tarehe 29 mwezi wa kwanza 2016
Akizungumzia Filum hiyo inayofanya vizur sokoni NISHA alisema Filum hiyo imemfanyia maajabu kwa kufanya vizuri sokoni kuliko alivyo tarajia.
Filum ya KIBOKO kabisa ni filum iliyotazamia mambo yanayotokea katika shule za mabweni ikiwa ni wazazi kusahau kufuatilia watoto wao wakidhani mabwenini ni mahala salama.. kumbe ni fikra potofu...
FILUM ya KIBOKO KABISA imeweka bayana yale yote mabaya yanayotokea katika shule hizo huku ujumbe ukifika kama ulivyopangwa na kwa aina yake..
FILUM hiyo amewashirikisha wasanii kadhaa kama KING MAJUTO,BEN BRANKO,JENGUA,JADA,NEEMA WA 20 PERCENT.na CHIPUKIZI wengi waliofanya vizuri
KUNANI NA ERICOMONDI?
ERICOMONDI msanii wa vichekesho nchini Kenya anayefikisha sanaa yake kwa hadhira kwa njia za majukwaani PIa ni maarufu katika kipindi cha kuchekesha cha Churchill show kinachorushwa na KTN KENYA
Ukaribu wa NISHA na msanii huyo pendwa wa Krnya uliibua maswali kwa mwaandishi na kupelekea kumtafuta NISHA afafanue hilo
"tunategemea kufanya kazi pamoja na ninadhani inaweza kua ni kazi inayofuata baada ya KIBOKO KABISA na hii itakua ni zawadi kwa mashabiki wa Afrika Mashariki hivyo wakae mkao wa kula " alisema NISHA.
..
..
..
ERIC amekua akifanya vizuri katika kazi zake za kuchekesha pia alijizolea umaarufu pale alipokua na kampeni ya kumkaribisha raisi wa Marekani Barack Obama alipokua anaitembelea Kenya ..
mbali na kuchekesha ERIC amekua akiijihusisha na kuimba katika uhalisia huo wa uchekeshaji
ERICOMOND katika ubora wake
...
...
KIBOKO KABISA
Filum ya kiboko kabisa bado inapaTikana madukani kote kwa part zote mbili.. Nisha alisema kwa anaehitaji odder ya Filum hiyo anaweza kupiga namb 0769089812 kwa odder au wakala yeyotewa STEP INTERTAINMET waliosambaa nchi nzima kwa jumla na reja reja.
...
...
..
...
..
NISHA MPAKA KUA BALOZI
SALMA JABU NISHA hivi punde ametawazwa kua balozi wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Tanzania
Akizungumzia wadhifa huo ambao anasema ni Kudra za Mungu na kufanya akabidhiwe sio kwasababu ya umaarufu wake ila kujitolea na kutowasahau watoto hao ..hasa katika vipindi kadha wa kadha amekua ni chachu kwa wasanii wenzake katika kuwakumbusha hasa alipotumia muda mwingi kutembelea vituo vya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
NISHA aliendelea kusema kua nyadhifa hiyo ya Ubalozi ataitumia ipasavyo kushawishi na kua sauti ya watoto hao kwani ni idadi kubwa ya jamii ambayo haina sauti na sauti ni watu kama yeye...
Alimalizia na kusema .. wasanii wasijisahau na kazi zao pia wakumbuke wanachokipata kugawana kwa asilimia chache na jamii ya wasiojiweza wakiwemo watoto waishio katika mazingira magumu.
Comments
Post a Comment