ZAWADI KWA NISHA

ZAWADI KWA NISHA.

PART 2

maisha yalikua chungu hasa kwa hii historia ya mama.aliokua ananipa..kila tulivyokua pamoja nilijihisi nahitaji msaada wa mtu wa tatu ambae amebaki historia nae ndio baba yangu mpenzi.....
.....hali ya mama ilizidi kubadilika ilifika kipindi ilinipasa niache shule..kulingana na tabu aliokua akiipata mama....
..nilipata shauku sana yakutaka kujua storia ya baba..ila niliogopa kumueleza mama animalizie hadithi kutokana pindi  alipomtaja baba presha ilimpanda...nilisema na moyo wangu...huku nikimtizama mama kwa roho ya huruma..
...
...
Siku moja NISHA yupo katika pirika za kutafuta kuni ili akapate kumpikia mama yake... Alimuona mtu mwenye mwili mkubwa mandevu yalimshamiri mithili ya @mwarabu_fighter alipanda hewani kisha alitisha...sura
Alimuona akija katika njia ile ile aliyokua anarudia nyumbani
NISHA alipunguza mwendo.na mwendo wa jitu yule ulimtisha NISHA.. alitoa macho kwa ishara ya kuogopa.....
Akautupa mzigo wa kuni chini nakukatisha porini mbio...
(Ilisikika sauti ya NISHA)
Kwakeli nilimuogopa mtu yule pengine labda ni ushamba wangu wa kijijini ila alikua tofauti...nilimtizama hadi anapoishia nikagundua hayuko peke yake walikuja wengi na gari kutoka mjini kwani walikua wamepaki gari lao maeneo yaleyale....
Nilisogea nikataka kushuhudia walitafuta nini.. Walionekana watu kadhaa waliovalia suti zao waliokua kama wanajadili kitu... kwa mbali NISHA slijificha ili ashuhudie watu hawa waliopendeza wengine walikua wanene wanene walikua wana kazi gani........
...
.....
Yalikua idadi ya magari mawili ila pembeni waliweka  hema ambalo lilizungukwa na watu wenye miraba minne kama wa tatu.. ila katika hema lile lilikua na watu waliokua wanaingia na kutok ila walivalia nguo za udaktari wa operesheni...
....
...
Walimaliza shuhuli yao na kukunjA hema lao na kuondoka....
.
..
..nilipata Shauku ya kusogea pale baada ya wao kuondoka... nilifika pale lilipokua limesimikwa hema niliona damu nyingi chini ..sikuitambua ilikua ni damu ya nn wakati ule... RIYAMA  alimsikiliza NISHA kwa ukaribu sana na alitaka kujua nini kiliendelea... Nini kinaendelea...

Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA