GAMBA MTAMU ANAEKUJA KUIBADILISHA TASWIRA YA MUZIKI WA BONGOFLAVER
NA MUANDISHI
mudi bellino
ISSA SHABANI MAVURA (GAMBA MTAMU)
msanii wa muziki wa Tanzania maarufu kama
Bongoflava, Ambae aliwika na kibao cha Maiyo
alichokifanya kwa projuza Tris. Daresalam. Baada ya kibao hicho GAMBA hakulaza damu akachomoka na kibao chake
kipya ambacho ndicho kilicho fanya Sweetstoryz blog
kumtafuta.GAMBA knachotambulika kama YOBORA.
YOBORA ni nyimbo ambayo imemfanyia mapinduzi sana GAMBA
kibao kilichofyatuliwa katika studio mpya zinazomilikiwa na
prodyuzer anaekuja kwa kasi anae julikana kwa jina la Cyrus.
Studio hizo zipo katika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
GAMBA hakusimama peke yake katika YOBORA amemshirikisha
Top B msanii pendwa mkoani KILIMANJARO.
GAMBA MTAMU
Blog ya sweetstoryz ilitaka kujua undani wa safari ya Gamba mpaka Moshi Mkoani
KILIMANJARO kumtafuta SYRUS.
"mimi Moshi ni nyumbani kabisa ila nimekua
nikitoka katika mipaka ya mkoa huu katika
kutafuta ngawira na ramani ya kuweza kutoka
kimaisha na muziki pia kwani nimekuja kufanyia
au kutolea mziki huu katika studio za nyumbani
kwani naamini nitapofanikiwa mimi nitakua
nimefanikisha na studio za nyumbani na kutangaza vya nyumbani,tofauti na ningeamua kufanya kazi na
studio maarufu za mbali na nyumbani. Japo sisemi kua sitofanya nao ila ni vizuri kuanzia nyumbani"
Alisema GAMBA MTAMU katika mahojiano na Blog hii.
AVUTIWA NA MB DOG
GAMBA akisema katika safari yake ya kimziki
amevutiwa sana na Msanii MB DOG hivyo kumpelekea GAMBA kuupenda mziki.
mbali na GAMBA msanii kongwe MB DOG amekua kivutio kwa wengi hasa sauti yake ambayo ilishika nyoyo za watu.
MB DOG KTK POZI
GAMBA amewataka shabiki pendwa wa mziki wa Tanzania wampokee na yupo wazi katika kupokea ushauri kupitia numb za blogger.. pia ameweka wazi kua ana usongo wa kubadilisha mziki wa Tanzania uwe wa pekee na unaotambulika kmataifa kwa hali ya upekee na uhalisia wa kitanzania...
UKITAKA KU DOWNLOAD YOBORA BY GAMBA MTAMU FT TOP B...
INGIA HAPA CHINI
(C)2016
BLOG OF THE PEOPLE, OF THE PEOPLE WE ARE THE PEOPLE MAKE PEOPLE NEWS
TANGAZA NASI HAPA BURE
JE WEWE NI MSANII
UNATAKA KUJITANGAZA
CALL/WASSAP 0656278685
Comments
Post a Comment