KUTANA NA MBUNGE ALIETUMIA VIDONGE VYA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME KAMA RUSHWA YA KUJIZOLEA KURA KATIKA UCHAGUZI
Atumia vidonge vya nguvu za kiume kuzoa kura
15 April 2016
Atumia vidonge vya nguvu za kiume kuzoa kura
Katika mataifa mengi ya Afrika wakati wa uchaguzi wanasiasa hutoa pesa ilikuwashawishi wapigaji kura kuwachagua.
Lakini huko Korea Kusini amini usiamini, polisi wameanzisha uchunguzi baada ya kuibuka madai kuwa wapiga kura wenye umri wa makamo walimpigia mwanasiasa fulani eti kwa sababu aliwapa vidonge vya kuongeza nguvu za kiume!
Yamkini mwanasiasa mmoja aliwashawishi watu hao wenye umri wa makaomo kwa kuwapa vidonge.
Mbunge wa eneo hilo la Suwon iliyoko karibu na mji mkuu wa Seoul ndiye anayetuhumiwa kwa njama hiyo.
Suwon ilishuhudia upinzani mkali katika uchaguzi uliofanyika Jumatano iliyopita.
Mbunge wa eneo hilo la Suwon iliyoko karibu na mji mkuu wa Seoul ndiye anayetuhumiwa kwa njama hiyo.
Jina la mshukiwa mkuu halijatajwa hadi ushahidi utakapopatikana.
Hata hivyo uchunguzi wa msingi umethibitisha kuwa mgombea huyo alikuwa na kiwango kikubwa mno cha madawa ya kuongeza nguvu za kiume kwa wakati mmoja.
Haijabainika ni kwanini wala alikusudia kuwapa kina nani.
Uchunguzi bado unaendelea.
TANGAZA NASI HAPA
KAMA WEWE NI MSANII CHIPUKIZI UNATAKA PROMO
0656278685
Comments
Post a Comment