Skip to main content

MOTO WATEKETEZA MADUKA KAGERA



BREACKING NEWS!!!
MADUKA YATEKETEA MOTO KAGERA

  • Moto mkubwa umezuka na kuteketeza vibanda vya maduka zaidi ya 150 katika mji wa Kayanga wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera magharibi. Moto huo ambao ulianza jana majira ya saa 2:00 usiku umeteketeza mali na bidhaa za aina mbalimbali kama mchele, sukari, nguo, simu, pamoja na bidhaa zingine.
    Gloria Kilio ambaye alikuwa akiuza vyakula vya nafaka, amesema stoo zake zote tatu (3) za nafaka zimeungua, “Stoo zilikuwa na magunia ya unga, mchele na sukari lakini vyote vimeteketea,” amesema Gloria huku akilia. Anasema wakati moto unatokea alikuwa tayari amekwisha kwenda nyumbani na kuwaacha wafanyakazi wake wakimalizia kufunga vibanda.
    Wafanyabiashara wengi wanasema walikuwa na mikopo na wengi wao hawana bima ya mali zao. Jonasi Nyarugenda ni miongoni mwa wafanyabiashara hao: “Moto umeteketeza stoo zangu nne zenye bidhaa mbalimbali kama sukari, mchele, ngano na mafuta,: anasema Jonas na kuongeza, “kwakeli ukitathimini kwa haraka siyo chini ya milioni 45 zimepotea.” Amesema kwamba alikuwa hana bima katika mkopo wake wa milioni 20 kutoka katika benki. 
    Hasara hiyo kwa kiasi kikubwa imechangiwa na ukosefu wa vifaa vya kuzima moto. Wananchi wa Karagwe imewapasa kusubiri gari la Zimamoto kutoka Bukoba Mjini (magari ya uwanja wa ndege) ambako ni kilomita 120 kufika karagwe mjini. Hata hivyo magari hayo yalikuta maduka mengi yamekwishateketea.



    chanzo
    clouds


Comments

Popular posts from this blog

MAHABA ZONE

ORODHA YA WANAUME WA WEMA YAFUNIKA KIMATAIFA

JIKE DUME HILI HAPA