Wema Isaac Sepetu ‘Madam’. DAR ES SALAAM: Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ (27), ametimiza miaka 10 ya ustaa wake tangu alipotwaa Taji la Miss Tanzania, mwaka 2006 hadi mwaka huu 2016 ambapo upande wa pili wa maisha yake ya kimapenzi ulibebwa na mtungo wa wanaume alioingia nao kwenye uhusiano, Amani lina ripoti kamili. Wema aliyezaliwa Septemba 28, 1989 akiwa mtoto wa mwisho kati ya mabinti wanne kwenye familia ya marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu kwa mkewe, Miriam Sepetu, mbali na ulimwende, pia ametikisa kwenye sinema za Kibongo, matangazo na runingani huku akipendwa na sehemu kubwa ya jamii. ….Akiwa na Idris. Wema mwenye sauti ya kitoto miaka yote, aliibuka kidedea kwenye Miss Tanzania mwaka huo akiwagaragaza Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Lisa Jensen. AANZIA KWA MR BLUE, TID Maisha yake ya kimapenzi ya awali, Wema alidaiwa kuwa ‘klozi’ na mastaa wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue’ na Khaleed Mohamed ‘TID’ kabla ya kuingia kwenye uchumba rasmi na aliyekuwa staa wa Bongo Movies, ma...
Comments
Post a Comment