DAIMOND , ROMYJONS BIFU ZITO
Exclusive: Bifu zito kati ya Diamond na Rommy Jones Diamond Platnumz vs Rommy Jones Kuna bifu kubwa linaendelea chini chini kati ya Diamond Platinumz na binamu yake na mtu wake wa karibu Rommy Jones. Chanzo cha bifu hilo japo wenyewe hawataki kuweka wazi inasemekana ni kitendo cha Diamond kumwambia Rommy aweke utaratibu wa kujitegemea yeye mwenyewe alafu yeye atamsapoti. Inasemekana Rommy hakufurahi kaona kama kadhalilishwa, kumbukeni Rommy hajui ata bei ya viatu kila kitu anawezeshwa na Diamond. Wengine wanasema chanzo ni Zari inasemekana Rommy ambae ni swaiba wake na Wema alikuwa anajaribu kumshawishi kwa muda mrefu Diamond arudishe mapenzi kwa Wema huku akisaidiwa na Aunt. Hii ilimuuzi sana Diamond maana Diamond kwa sasa jicho lake lote lipo kwa mwanae Tiffa na mpenzi wake Zari sasa kuona mtu wake wa karibu anamshawishi kuvuruga furaha yake ikaleta doa kwenye uswahiba wao. Kingine ni ishu ya Wasafi records label mpya ya Diamond ambayo kawekeza pesa ndefu lakini kampa usimamizi ndugu...