Posts

Showing posts from September, 2015

LINEX AMRUSHIA MADONGO IZO BIZNESS... AMPA ONYO KALI

Image
Linex Mjeda aka LINEX .. mkali wa sauti za mchanganyiko wa lafudhi za ki magharibi... Ameingia katika Tifu zito na Msanii IZO mzee wa BIZNESS (BISHOO) .. anae tamba kwa ngoma kadhaa na mashairi ya kusifika... Kichwa hicho kutoka Mbea kimekua kikisumbua sana katika Uwanja wa mziki Mgumu maarufu HIP HOP ya BONGO..... Msanii pekee aliowahi kumtaja mtoto wa Raisi na kumuambia aufikishe ujumbe kwa Muheshimiwa nyimbo iliotambulika kwa jina la Ridhiwani ni nyimbo ambayo ilimueka IZZO katika dira ya biashara ya mziki aufanyao .. .. MADONGO YA LINEX Kukaa kimya kwa IZZO kumezua kishindo kikubwa sana kwani anatarajia kuingia katika chart na ngoma yake ambayo inazungumziwa na watu wengi ngoma ambayo haijatoka bado inayotambulika kwa jina la SHEMEJI LAKE ngoma ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni... Kwa hali ya utani LINEX alimtania IZZO na kumtaarifu kua anataka kujua maana ya hiyo nyimbo anaogopa isije kua shemeji ki vingine akashindwa kumkaribisha nyumbani kwake... Wasanii hao wameku...

NISHA,BARAKA DE'PRINCE WABAMBWA LIIIVE ,NISHA AIKIMBIA AIBU AJIFICHIA CHINA (MAMBO HADHARANI)

Image
Msanii SALMA JABU (nisha) wa Bongo Muvie ambae sasa yupo katika chart za wasanii wa kike wanaofanya kazi nzuri katika Tasnia ya Filamu TANZANIA.... Hivi karibuni ameingia  katika sintofahamu na minong'ono dhidi yake yeye na Msanii wa Tuzo ya Msanii Bora anechipukia (KTMA) BARAKA DE PRINCE .. ... MAMBO HADHARANI lisemwalo lipo kama halipo basi lipo njiani tena karibu sana.. kutokana na siri kua sio siri wasanii hawa waliona waweke mambo hadharani baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kuwaambia watu au watu kutofahamu... Wasanii hawa walionekana kukubaliana sana na kusifiana hadharani swala ambalo sio la kawaida kwa wasanii wetu... Matukio haya hua yanajirudia miongoni mwa wasanii kadhaa husifiana mwisho wasiku hufanya kweli (NEY na SHAMSA)... walionekana wakitupiana katika kurasa zao na sifa kedekede kati yao mwishoniiii...?? .. .. MINONG'ONO Upele umewapata wakunaji... wale wakali wa kufuatilia SKENDO jijini walifungua masikio na macho kufuatilia baadhi ya maneno ya...

SAA YA HAMIS KIIZA YAVUNJWA TAIFA

Hatimaye ile raha iliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki weng nchini imetimia ambapo Mechi kati ya watani wa  jadi simba vs yanga kuchezwa jana  jion  katika uwanja wa  taifa  ya timu ya yanga kuibuka na  magoli mawili na  point Tatu muhimu, katika mchezo ambao simba walianza kutawala iliwachukua dakika 44 yanga kujielewa na  kuandika bao la kwanza lililofungwa na  mchezaji wa  zaman  wa  simba Amiss Tambwe na  kushindiliwa goli la pili katika kipindi cha pili na Malimi Busungu na  kuvunja ule  mchezo uliokuwa ukioneshwa na  Hamis  kiiza katika michezo iliyopita ya kuonyesha kwamba muda  wanao kwa ishara ya kushika mkono akionesha saa  bado zipo kwani Jana alikuwa chini  ya ulinzi mkali wa  cannavaro na  kelvin yondani kwa mantiki hiyo Yanga ya Dar es salaam imeendelea kushika usukani wa  ligi hiyo ya Tanzania bara alimaarufu kama VPL.

SIMON MSUVA HUYOOO SIMBA

Baada ya kuhujumiwa katika mechi  kadhaa akiichezea yanga dhid ya simba  hatimaye atolewa tena  katika kipindi cha kwanza cha mchezo kati ya simba vs yanga hapo jana  kati msuva ambaye  siku zote  amekuwa akiambiwa hachezi vizur kabisa pindi wanapokutana watani hao wa  jadi na  kudhaniwa kuwa  yy anaipenda club ya simba  bado hajatoa tamko lolote kuhusu tuhuma hiyo kumbuka msimu uliopita mashabiki wa  klabu ya yanga walimzunguka wakitaka kumpiga kwa kile  kilichodaiwa kuwa  n kucheza vibaya dhid ya simba hivyo  kuna  uwezekano mchezaji huyo akawa pande hiyo ya rangi  nyekundu na  nyeupe msuva ambaye jana  alilazimika kutolewa baada ya kuonyesha kiwango kibovu na  nafas yake kuchukuliwa na  Malim Busungu ambaye aliipatia Yanga bao la ushind hongera yanga kaza but simba

BRENDAN RODGERS APEWA SIKU KUMI TU LIVERPOOL http://bentheshilohsport.blogspot.com/2015/09/brendan-rodgers-apewa-siku-kumi-tu.html

YONDANI ANENA ASEMA KIIZA WAO HUKO HUKO

Image
Ni vita ya soka kati ya watani wa jadi wa  Tanzania Simba itakayokuwa mwenyeji dhidi ya dar es salaam yanga Africa siku ya jumamosi katika uwanja wa taifa  tayari simba  ipo  mjini  unguja katika kujiwinda na  mechi hiyo inayotazamiwa kuwa  Kali kwa pande  zote mbili kwa upande wa  yanga beki wake Kelvin yondani amesema siku hiyo atahakikisha mkali wa  mabao kwa sasa  katika ligi ya vpl Hamis kiiza haisumbui kabisa ngome yake  ya ulinzi yanga inajivunia beki yake  hasa ya kati kwa kucheza kwa muda mrefu na maelewano mazuri huku simba nayo ikijivunia safu yake maridadi ya ufungaji yanga itateremka dimbani siku ya jumamosi ikikumbuka mchezo wao wa  mwisho ambapo simba ya dar es salaam iliibuka na ushindi timu zote mbili zipo  visiwani huku yanga ikiifuata simba  unguja ikitokea Pemba je nani ataibuka mshindi mshindi tusubiri jumamosi ya wiki hii

NISHA KUNUKIA CCM.... MAKADA WAPANDA DAU

Image
Msanii wa Filum za Kibongo nchini SALMA JABU NISHA... anaesifika kwa kua ni moja kati ya wanawake wachache Hapa nchini ....kwa kujituma na kua wabunifu hasa wanapoonekana wakipambana wakitumia vipaji vyao kuinua maisha yao... Katika kipindi hichi cha kampeni na mbio za kukimbilia Uchaguzi mkuu wa maraisi ..madiwani na wabunge kumetokea  nenda rudi ya wasanii kujigawa kwasababu ya itikadi ya vyama huku kupelekea wasanii hao kunadi vyama ambavyo walijihusisha navyo.... WASANII WAJIGAWA. wakati kampeni zikizidi kuchanja mbuga huku kila chama kikinadi sera zake ... ilikua hivyo hivyo katika makundi ya wasanii waliopo katika vyama hivyo.. Vyama vikuu ambavyo vimo katika ushindani mkubwa ni CCM na vyama vilivyo unda umoja almaarufu UKAWA.. Wakati CCM ikimnadi mgombea wake wa Uraisi kupitia tiketi ya chama hicho DK JOHN POMBE MAGUFULI... Huku UKAWA wakimnadi mgombea uraisi.kupitia chama hicho MH EDWARD NGOYAI LOWASA. moto huo ulikolezwa na makundi ya wasanii ambayo yanasindikiza kam...

LOWASA,MSINDAI.. WANADI CCM JUKWAA LA UKAWA

Image
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassajana alizua sintofahamu baada ya kusema; “CCM oyee”, kauli iliyowafanya wananchi hao kukaa kimya na walipoona akicheka waliitikia “oyeee” huku nao wakicheka na kumshangilia. Ingawa ilitokana na ulimi kuteleza, yeye mwenyewe alisema alitamka neno CCM kama utani ili kubaini ni wananchi wangapi wanaokishabikia chama hicho kati ya waliojitokeza uwanjani hapo kumsikiliza wakati tayari amekwishaeleza jinsi chama hicho tawala kilivyoshindwa kuliletea taifa maendeleo. Msindai kama Lowassa Wakati Lowassa akieleza kwamba alisema hayo kwa utani aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Mgana Msindai aliyekihama chama hicho na kujiunga na Chadema, alitoa mpya baada ya kukiombea kura chama chake hicho cha zamani badala ya Ukawa kwenye mkutano wa hadhara. Msindai alitoa mpya hiyo juzi jioni wakati akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni...